Picture1-swahili
Watanzania waendelea kufaidika kutoka kwa hospitali ya Apollo iliyoko nchini India. Hii ni kufuatia hosiptali hiyo kufanikiwa kuwatenganisha mapacha wa kike Abriana na Adriana waliokuwa wameunganika chini ya kifua na tumboni kutoka nchini Tanzania katika upasuaji uliofanyika tarehe 17 Novemba 2014 nchini India. Mapacha waliounganika kwa mtindo huu hujulikana kwa watalaam kama Thoraco Omphalopahus na upasuaji uliofanyika na hospitali Apollo ulikuwa wenye mafanikio na wa aina yake.
Mapacha Abriana na Adriana awali ya upasuaji huo walikuwa wameunganika kuanzia chini ya kifua na tumbo, hali kadhalika walikuwa wakitumia mvungu mmoja wa moyo na maini yaliyounganika.  Changamoto ya upasuaji wa mapacha hawa kwa madaktari ulikuwa kufanya utenganishaji bila kuwavujisha damu nyingi ambayo waliweza kukabiliana nayo ipasavyo kutokana na madaktari waliokuwepo wenye wataalum wa kiufundi na matibabu.
Upasuaji huo ulifanywa na jopo la watalaamu 50 waliobobea katika taaluma mbali mbali za tiba ya afya ya kabla na baada ya upasuaji ambao uliendelea kwa masaa 11.  Watalaamu walifanikiwa kutenganisha viungo vilivyo kuwa vimeungana lakini mapacha hawa walipona na kupata ahueni kwa haraka hivo kusaidia zoezi zima la uponyaji baada ya upasuaji.
Picture2-swahili
Hali kadhalika, hatua nyingine ya muhimu katika upasuaji huo ilikuwa kurudisha viungi husika katika mahala pake baada ya kuvitenganisha. Akizungumzia kuhusu hili Dkt. K S Sivakumar Plastic & Reconstructive Surgeon anasema, “Baada ya upasuaji, moyo wa moja ya mapacha ulitakiwa kurudishiwa mahali pake ili kuzuia mbenuko na uharibifu pamoja na maini yaliyokuwa yameungana. Ilichukua majopo mawili ya wataalum kwa masaa nne kukamilisha ufungaji wa maini, moyo, na utumbo katika mahala pake.”