Jana Bungeni Mbunge wa viti maalum CCM mh. Kwegir (Samahani kama nimekosea kuandika jina lake) alitoa machozi kulalamikia jinsi maalibino wanavyodharauliwa. Alililalamika kuwa mauaji ya maalibino yanaengelea kutokea bila hatua za dhati kuchukuliwa kwa kuwakamata wahusika wakuu. Alilia kuona kuwa faru aliyeuawa Serengeti hatua kali zilichukuliwa mara moja. Je hao faru wana thamani kuliko maisha ya maalibino?

Mimi binafsi najiuliza, je serikali yetu inawajali wananchi wake na sii kwa maalibino tu? Ninauliza hivyo maana wale waliowapora wazungu huko Serengeti wamekamatwa mara moja. La kushangaza mpaka sasa shambulizi la mbunge wa ilemela na wa ukerewe bado ni tata, mauaji ya maalibino wengi waliohusika hawajakamatwa, tumesikia kukatwa mapanga kwa akina mama huko kanda ya ziwa na sasa utekaji na kuumizwa vibaya kwa Dr. Ulimboka.


Je, Serikali ya CCM inawathamini zaidi usalama wa wanyama na wageni na kuwapuuza raia wake?