,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Tuesday, August 30, 2016


barafu

barafu JF-Expert MemberHii ndio moja ya ndege mpya ya Air Tanzania iliyo tayari kwa kila kitu.Hapa ipo kwenye Hangar(eneo la matengenezo ya ndege) nchini Canada tayari kwa kuanza safari ya kuja Tanzania.Wakati wowote na siku itakayotajwa ya mwanzoni mwa mwezi September ndege hizi mbili zitatuwa katika uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dsm.


Katika picha ni ndege hiyo ikiwa na rangi ya ATCL na picha nyingine ni kabla ya kuwa na rangi yoyote ya kampuni na nembo.Nchini Canada ndege hiyo imepewa Reg # ya C-FIFG...kwa mujibu wa ICAO kila nchi huwa na usajili wake tofauti,mfano kwa ndege zote zilizosajiliwa Kenya lazima zianze na 5Y-(then hufuata herufi za ndege husika ambazo hazitafanana na ndege nyingine yoyote)-,ndege zilizosajiliwa Uganda huanza na 5X-..ndege zenye usajili wa Afrika Kusini huanza na ZS- na hivyo ndege zenye usajili wa Canada huanza na 5H-,nilitembelea Kigali,wao huanza na 9XR-..

Hivyo ndege hii ambayo Tanzania imenunua huko Canada ilitambulika kwa usajili wa C-FIFG,na hivyo itakavyotua Tanzania itabidi tubadili na tuipe usajili wa Tanzania utakaoanza na 5H- .

Kwa hili nimpe hongera Rais Magufuli na Serikali yake,kwani hakika ukiangalia historia ya ndege hii ina mwaka mmoja tu toka ianze kutengenezwa kiwandani.Lakini pia ukiangalia flight movement records zake inaonyesha imeruka Mwezi August 2016 kwa muda wa saa moja na dakika tisa kama sehemu ya majaribio.Hii ni dalili kuwa tunaenda kuwa na ndege mpyaaa,ingekuwa enzi za ujana wetu miaka ya 80 tungesema "ndege mmaaaaaa"!!PONGEZI KWA SERIKALI HII YA AWAMU YA TANO.

Nimeambatanisha "details" za ndege hiyo,ambapo ili watu wasione tumeingizwa chaka bado ina Reg# ya Canada ambayo sisi tutaibadilisha vile tunavyotaka.Hakika ndege hizi ni rafiki kwa mazingira ya viwanja vya Tanzania na usafiri wa ndani.Itasaidia kutua hata katika viwanja "korofi" kama Mtwara,Kigoma,Tabora,Iringa,Songea,Dodoma(japo nasikia inafanyiwa ukarabati) na viwanja vingine kama Arusha,Mwanza,Znz,Tanga na Mbeya.
WELCOME TO THE MARKET ATCL.....THE WINGS OF THE KILIMANJARO
image.jpeg image.jpeg image.jpeg image.jpeg image.jpeg


#Prof Mbarawa: Rais Magufuli amedhamiria kuleta HapaKaziTu ya kweli katika sekta ya miundombinu;

#Prof Mbarawa: Sekta hii imetengewa zaidi ya Sh. Trilioni 4 ambapo Bil 500 ni maalum kwa ajili ya kufufua Shirika la Ndege;

#Prof Mbarawa: Tumeanza kutekeleza ahadi ya kuwapatia meli kubwa na ya kisasa Ziwa Victoria.Tenda inafunguliwa;

#Prof Mbarawa: Reli ya kiwango cha Standard gauge itajengwa kwa mtindo wa wakandarasi tofauti ili imalizike haraka;

#Prof Mbarawa: Tutaboresha eneo na kivuko cha Kigamboni? Ukarabati wa vivuko unakamilika..tozo za daraja tumepokea maoni mapya ya wadau tutayafanyiakazi;

#Prof Mbarawa; *Shirika letu la ndege ni kama lilikuwa limekufa..sasa tunalifufua*;

#Prof Mbarawa: Ndege mbili mpya za kwanza aina ya *Bombadier Q400 zitawasili Dar Sept. 19, 2016*;

#Prof Mbarawa; Tumenunua ndege hizi zenye usalama mkubwa, uwezo wa kutua popote nchini hata kwenye viwanja vyenye changarawe tu au vyenye eneo dogo tofauti na ndege nyingine na zinatumia mafuta kidogo sana;

#Prof Mbarawa: *Kwa kununua moja kwa moja kwa watengenezaji tumetumia USD mil. 23.5 kwa kila moja wakati bei ya sokoni ni USD mil. 31 kwa ndege moja*;

#Prof Mbarawa: *Tumeanza kuboresha viwanja vya ndege Dodoma, Mwanza, Kigoma* na kwingineko. Lengo ni mikoa yote nchini kuwa na viwanja vya ndege vyenye kiwango cha lami ndani ya miaka minne ijayo;

#Prof Mbarawa: Kuhusu Bandari tunaendelea kuboresha ushindani wa kibiashara na kuongeza mapato;

#Prof Mbarawa: Nimeagiza wafanyakazi wote wa Bandari waliohusika kufunga mifumo ya chini ya kiwango ya TEHAMA huko nyuma wachukuliwe hatua;

#Prof Mbarawa; *Nimeipa Bodi ya Bandari lengo la kukusanya Sh. Trilioni 1 mwaka huu wakishindwa bila sababu nitawaonesha mlango wa kutokea*;

#Prof Mbarawa: Tunakwenda kuifanya kampuni ya simu nchini kuwa bora zaidi.Tumeshawalipa Airtel hisa zao sasa tunaimiliki TTCL kwa asilimia 100;

#Prof Mbarawa: Tuliwatengea ruzuku makampuni ya simu kuweka minara ya simu mikoani wakashindwa kutekeleza...tumeleta Viatel wamejenga mtandao mkubwa na sasa mawasiliano ya simu vijijini yamekuwa bora zaidi nchini;

#Prof Mbarawa: Nia yetu ni kuifanya sekta ya miundombinu na mawasiliano kuwa chachu ya kuifikia Tanzania ya viwanda.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi