,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Sunday, August 21, 2016

_90842334_hi033706107
Daraja refu zaidi duniani ambalo sakafu yake ni kioo litafunguliwa katika mji wa Zhangjiajie katika mkoa wa Hunan nchini China wikendi hii.

Daraja hilo ndilo la juu zaidi lenye sakafu ya kioo duniani na linaunganisha milima miwili ambayo hufahamika kama Milima ya Avatar. Filamu ya Avatar iliandaliwa katika milima hiyo.
Ujenzi ulikamilika Desemba mwaka jana. Urefu wa daraja hilo ni 430m na liligharimu $3.4m (£2.6m).
Daraja hilo limewekwa 300m juu ya ardhi, kwa mujibu wa shirika la habari la serikali la Xinhua.
Sakafu yake imeundwa kwa vipande 90 vya vioo ambavyo vina tabaka tatu.
Kwa mujibu wa maafisa wa serikali, daraja hilo lenye upana wa mita 6, ambalo mchoro wake uliandaliwa na msanifu mijengo kutoka Israel Haim Dotan, tayari limeweka rekodi kadha za dunia katika usanifu mijengo na ujenzi.
Hili ni suala kuu. Lakini maafisa wameandaa hafla za kudhihirisha uthabiti wake. Maafisa walituma watu wenye nyundo kujaribu kuvunja vioo. Pia magari yaliyojaa abiria yalipita juu yake mapema mwezi huu.

zsb

slide_430268_5583440_free - Copy

slide_430268_5583438_free - Copy

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi