,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Tuesday, August 23, 2016

Mkuu wa kitengo cha masoko na mawasiliano Vodacom, Nandi Mwiyombella akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya kuidhamini Efm kwasababu ni sehemu ya kuwafikishia muziki wateja wa vodacon leo jijini Dar es Salaam.
Meneja Mkuu wa Efm, Denis Ssebo akizungumza na waandishi wa habari (hapo pichani) juu ya tamasha la kila mwaka lijulikanalo kama muziki mnene ambalo litaanza rasmi Agosti 28 mwaka huu katika eneo la Boko leo jijini Dar es Salaam.
(Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii).
REDIO ya burudani ya Efm imezindua tamasha la kila mwaka kijulikanalo kama muziki mnene ambalo litaanza rasmi Agosti 28 mwaka huu katika eneo la Boko.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Meneja Mkuu wa Efm, Denis Ssebo amesema tamasha hilo litafanyika kwa kipindi cha wiki 12 sawa na miezi mitatu ambapo muziki utapigwa katika bar 12 za vijijini vya Dar es Salaam na Pwani ikiwa na kauli mbiu isemayo 'Tunasepa na kijiji '.
Alisema mziki mnene mwaka huu itaenda sambamba na kampeni ya nje ndani ambapo vipindi vinne vitarushwa moja kwa moja katika mtaa husika kwa siku nne mfulukilizo.
Ssebo alivitaja vipindi hivyo kuwa ni Uhondo ambacho itafanyika siku ya jumatano, Sports headquarters siku ya alhamisi, joto la asubuhi siku ya ijumaa na fonga mtaa siku ya jumamosi ambapo watapiga na burudani ya mziki wa singeli kwa lengo la kutafuta vipaji vya wasanii wa muziki huo.
Mkuu wa kitengo cha masoko na mawasiliano vodacom Nandi Mwiyombella alisema wanafurahi kuidhamini Efm kwasababu ni sehemu ya kuwafikishia muziki wateja wa vodacon
"Burudani ndio sehemu ya maisha ya kila mtu na lengo ni kuhakikisha kwamba wateja wetu anapata burudani ya muziki kupitia Efm,"amesema Nandi.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi