,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Friday, August 19, 2016


Kuna watu wameniomba niweke CV yangu hapa, naiweka kwa muhtasari tu!


Nizaliwa Mei 22, mwaka 1982 katika Hospitali ya Ocean Road ya Dar es Salaam. Nilipata elimu ya msingi katika Shule ya Msingi Ilala Boma na kuhitimu darasa la saba mwaka 1997 na kupata bahati ya kuchaguliwa kuendelea na masomo ya sekondari kidato cha kwanza hadi cha nne, katika Shule ya Sekondari Kibaha na kuhitimu kidato cha nne mwaka 2001. Mwaka 2002 nilichaguliwa kujiunga kidato cha tano Shule ya Ufundi Tanga, maarufu kama Tanga Technical School. Nilihitimu kidato cha sita mwaka 2004.

Mwaka 2005 nilichaguliwa kujiunga na elimu ya juu, katika Chuo cha Uhasibu Arusha, kusomea stashahada ya juu katika Sayansi ya Kompyuta (computer science) na kuhitimu mwaka 2008. Mwaka 2009 niliajiriwa kwa nafasi ya mchambuzi wa mifumo ya kompyuta katika Halmashauri ya Jiji la Arusha.

Mwaka 2011, niliajiriwa kama msimamizi mwandamizi wa mifumo ya kompyuta wa Chuo cha Kimataifa cha Nelson Mandela. Pia mwaka 2011 nilijiuzulu nafasi hiyo pale Chuo cha Nelson Mandela na kurudi Jiji la Arusha. Niliweza kurudi Jiji la Arusha kwa kuwa sikuwa nimeacha kazi, bali niliomba likizo bila malipo.

Baadaye niliendelea na safari yangu ya elimu na mwaka 2010 nijiunga tena Chuo cha Uhasibu Arusha kusoma shahada ya uzamili (masters degree) katika masuala ya uongozi na teknolojia ya habari na kuhitimu mwaka 2011.

April 2012 niligombea ubunge wa Afrika Mashariki na na kushika nafasi ya sita kati ya watu 81 tuligombea.

May 2012 niliteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Korogwe nafasi ambayo ninayo hadi sasa!

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi