,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

,.,.

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Tuesday, August 30, 2016Rais John Magufuli akiwa ziarani Singida kikazi alisisitiza tamko lake la kuzuia shughuli za kisiasa kwa wagombea walioshindwa kwenye Uchaguzi Mkuu uliopita na akasisitiza sana kwamba asijaribiwe kabisa kama Rais mpya. Lakini Tarehe 27/7/2016 mjini Dar viongozi wa Chadema walikutana na waandishi wa habari na kuelezea dhamira yao ya kutaka kufanya maandamano pamoja na mikutano maalum nchi nzima siku ya tarehe 1/9/2016 katika ngazi zote kuanzia msingini mpaka Taifani kwa kile wanachokiita Umoja wa Kupambana na dikteta Tanzania (UKUTA). Katika kilio chao hicho ambacho Rais Magufuli anachokiita ni cha kushindwa tu uchaguzi uliopita, kilidai kuwa kimsingi sababu ni jinsi wabunge wao wanavyozuiwa kufanya mikutano na wananchi, huku wakinukuu vipengele kadhaa vya Sheria ya Vyama vya Siasa, vinavyotoa haki ya kufanya mikutano ya kisiasa bila ya kusubiri kipindi cha Uchaguzi Mkuu.

Tarehe 28/7/2016 Msajili wa Vyama vya Siasa nchini chombo ambacho kikatiba ndicho chenye mamlaka na Vyama vya siasa nchini kilitoa tamko rasmi la kukemea kitendo hicho cha Chadema akinukuu Sheria namba (5) ya Jamhuri ya Mwaka 1992 kuhusu Vyama vya Siasa kifungu namba 9(2)(C) inayokataza Chama Chochote cha Siasa kutumia au kuhamasisha matumizi ya nguvu au vurugu kama njia ya kufikia malengo yake ya kisiasa nchini. Msajili alisema tamko la Chadema lilijaa lugha za uchochezi, kashfa, kuudhi na uhamasishaji wa kuvunja amani ya Taifa huku  kifungu cha 9(2)(f) kinakataza Chama chochote cha siasa nchini kuruhusu Viongozi au wanachama wake kutumia lugha ya matusi, kashfa, na uchochezi ambayo inaweza kusababisha au ikapelekea kutokea uvunjifu wa amani. Na kwamba Kanuni za Maadili ya Vyama vya siasa ya Tangazo la Serikali namba 215 la Mwaka 1977 pia inakataza Chama cha siasa kutumia lugha ya matusi, kashfa, uongo na uchochezi. Aliongeza kuwa Kanuni ya 5(1)(d) ipo wazi kwamba Vyama vyote vya siasa nchini vinatakiwa kutotoa maneno yoyote au maandishi ya uongo kuhusu mtu yoyote au chama chochote cha siasa. Msajili alisema anatumia Kanuni namba 6(2) ya Maadili ya Vyama vya Siasa kukuemea tamko la Chadema. Msajili pia aliweka wazi kwamba kuna uwezekano mkubwa wa chama hicho kuchukuliwa hatua za kisheria na Msajili.

Vyama vingine vya siasa pia vilijitokeza kutoa maoni yao kuhusiana na suala hilo la Chadema la kutishia kuvunjaa Sheria ya Jamhuri. Kwa upande wake CCM ilivitaka vyombo vya Dola yaani vya Ulinzi na Usalama wa Taifa kuchukua hatua zinazostahili kukabiliana na vitendo hivyo vya uvunjifu wa Sheria, “Tunaomba vyombo husika visisite kuchukua hatua zinazostahili bila kumuonea mtu lakini bila kufumbia macho vitendo vyenye lengo la kuwahujumu WaTanzania walio wengi walioamua kuchapa kazi kuitikia wito wa Rais na Serikali ya Awamu ya Tano ya kufanya kazi tu. Serikali haijazuia Wabunge kufanya mikutano ya siasa kwenye majimbo yao na haijakizuia chama chochote cha siasa nchini kufanya mambo shughuli zake kwa mujibu wa Katiba ya vyama nchini. Kwa pamoja Chama cha Wananchi (CUF) na NCCR-Mageuzi walisema kuunga mkono hatua hiyo iliyoitwa ni ya Kuvunja Sheria na Msajili wa vyama vya siasa nchini, huku wote vikidai kutohusishwa rasmi na Chadema kwa barua au taarifa za kiofisi kuhusiana na maandalizi ya shughuli hiyo. Lakini vyama hivyo vyote vimesisitiza dhamira yao ya kushiriki kwenye fujo na vurugu hizo iwapo vitahusishwa rasmi na Chadema.

Historia ya jambo hili inaonyesha jinsi nchi nyingi Duniani zilivyolazimika kutumia Sheria zao au kutunga zingine mpya kukabiliana na tatizo kama hilo la Chadema. Kwa mfano Tarehe 26/3/2016 Serikali ya Spain ilipitisha “Sheria ya Wananchi” ambapo yoyote atakaye andamana au kupinga Serikali atapewa adhabu na Polisi ya kulipa Dola za Kimarekani 30,000 mpaka 650,000 au kufikishwa kwenye Sheria na kufungwa Miaka 3. Nchini Canada katika Jimbo la Quebec Mwaka 2012 Serikali ya kule ilipitisha Mswaada mpya wa Sheria (Quebec Bill 78) ambao unapiga marufuku mkusanyiko wa zaidi ya watu 50 bila ruhusa ya Serikali kwa kulipishwa faini ya Dola kuanzia 5,000 mpaka 125,000 kwa wahusika. Mwaka jana Oktoba, Uturuki nayo ilipitisha Sheria ya kupiga marufuku maandamano au mikusanyiko ya kisiasa bila idhini ya Serikali. Nchi za Ufaransa na Australia pia nazo zimepitisha Sheria hizo mpya za kubana Maandamano na Mikusanyiko ya kisiasa Mwaka huu mwanzoni, huku Nchi za Misri, Ukraine, Mexico na Russia zikipiga marufuku kabisa vitendo hivyo kufanyika kabisa kwenye nchi hizo. Na hata Baba wa Demokrasia Marekani huko katika mji wa Baltimore, waandamanaji wote wa kifo cha Mweusi Friddie Gray aliyeuliwa na Polisi kwa makosa walikamatwa na kurudikwa Rumande kwa masaa 48 kwa kutokuwa na kibali cha maandamano kama hayo ya UKUTA yanayopangwa na Chadema tarehe 1/9/2016.

Kwa kumaliza ni kwamba hakuna mvutano wowote wa Kisiasa baina ya Chadema na Serikali isipokuwa kuna Chadema kuipima Serikali mpya ya Rais Magufuli, ni kawaida Duniani kila kunapokuwa na Serikali mpya kwa Vyama vya upinzani kuipima ipo tayari kwenda maili ngapi katika kutumia Sheria za Jamhuri kulinda amani ya Taifa. Ni matumaini yangu kwamba Chadema anatishia nyau tu lakini hawana hiyo nia ya kuvuruga amani ya Taifa letu. 

William Malecela aka Le Mutuz Nation #+255 717 618 997 

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi