,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Wednesday, August 31, 2016

Atembelea masoko yote ya wamachinga kujionea Kero 
Awatangazia Neema wamachinga kuingizwa soko jipya la Mwanjelwa Hakuna mmachinga atakayesumbuliwa kwa sasa mpaka miundombinu na huduma ziboreshwe masoko yote YA wamachinga  Atoa wiki mbili Tanesco na Mamlaka ya Maji kupeleka huduma soko la Nanenane
- Awajeshesha Kwa muda wafanyabiashara wa stendi wakati wakisubiri miundombinu kuboreshwa 
- Ni mkutano wa kihistoria mamia wajitokeza kueleza Kero wengi waupongeza utaratibu wa Mkuu wa Mkoa
MKUU wa Mkoa wa Mbeya leo amekutana na wafanyabiashara wadogowadogo ( wamachinga) kwa lengo la kusikiliza Kero zao na kuzitafutia ufumbuzi
MAMIA YA wamechinga wamefurika na kueleza Kero zao ikiwemo ukosefu wa vyoo, Maji , Umeme na stendi za kushushia abiria ktk maeneo kuwa ndiyo kikwazo cha wao kutoweza kukaa ktk masoko yao
Mkuu wa Mkoa ameagiza mamlaka YA Maji , Tanesco na jiji la Mbeya KUANZA mara moja uboreshaji wa miundombinu na huduma ktk masoko yote YA wamachinga
Katika kuhakikisha wamachinga wa mwanjelwa wanapata fursa amemwagiza Mkuu wa wilaya kushirikiana na jiji kuwaingiza wamachinga soko jipya la mwanjelwa
Aidha amewarejesha kwa muda wafanyabiashara wa stendi YA kabwe kwa ma sharti la kufanya biashara ktk mpangilio ulio mzuri na unaozingatia kanuni za usafi
Ameunda kikosi kazi cha watalaam wa jiji , afisa toka ofisi YA Mkuu wa Mkoa na madiwani wawili mhe Geofrey Kajigili na mhe Agnes Mangasila chini YA uenyekiti wa Mkuu wa wilaya kusimamia na kuratibu suala la kuboresha miundombinu na huduma YA masoko yote ya wamachinga
Amewataka wamachinga kutouza maeneo waliyopewa ni vema sasa wakayaendeleza na masoko yote yatakapoboreshwa wamachinga WOTE watatakiwa kufanya biashara ktk masoko hayo na si barabarani

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi