,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Friday, August 26, 2016

TUNDA43
WASANII wetu wana maisha f’lani ya kupritendi sana, wanaishi maisha ya kuigiza sana hadi wanakera. Kwa wafuatiliaji wa habari za mastaa wa muziki Bongo, watakuwa wanafahamu jinsi Video Queen Tunda Sabasita ‘Tunda’ alivyokuwa anajinasibu kuwa na uhusiano wa kimapenzi na rapa David Genzi ‘Young D’.

Alikuwa akifanya hivyo huku akitupia picha akiwa ‘close’ na jamaa huyo. Kwa kifupi walikuwa wakiishi kama wapenzi. Hata katika moja ya habari zilizowahi kuandikwa kwenye magazeti pendwa ilikuwa ni kuhusu mwanadada huyo kutangaza ndoa na Young D.
Alisema: “Ni kweli niko na D na ninampenda sana, Mungu akipenda tutakuwa mwili mmoja soon kwa sababu nimempima na kuona ndiye mwanaume mwenye nafasi kubwa kwenye moyo wangu.”
Cha ajabu sasa, baada ya Young D kutangaza kuacha kuvuta unga, kume-onekana kuna kitu kimewate-nganisha. Sasa ishu siyo kutengana kwao lakini majibu aliyoyatoa Tunda alipoulizwa kuhusiana na uhusiaono wa wao.
Hebu soma mahojiano hapa chini uone jinsi hawa wasanii wanavyozingua:
Showbiz: Vipi hujammisi mpenzi wako Young D?
Tunda: Young D ni msanii au?
Showbiz: Ina maana umemsahau au humjui na wakati alikuwa mpenzi wako wa kupika na kupakua?
Tunda: No! Hajawahi kupata nafasi hiyo?
Show-biz: Kwa hiyo leo unakana kuwa hamjawahi kuwa wapenzi?
Tunda: Simkani ila ndiyo ukweli wenyewe?
Showbiz: Mbona kuna picha ambazo nyingi mmepiga wote kama wapenzi?
Tunda: Picha napiga na watu wengi sana kutokana na muonekano wangu mzuri, kwa hiyo watu wengi hupenda kupiga picha na mimi.
Showbiz: Kwa hiyo unataka kuniambia hata hukumbuki kama mlipiga picha?
Tunda: Nakumbuka nilishawahi kupiga na huyo Young D lakini sikumbuki ni wapi na ni lini.
Ijumaa: Kwa hiyo hujawahi hata kusikiliza nyimbo zake?
Tunda: Mimi siyo mpenzi wa Hip Hop kabisaaa.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi