,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Sunday, August 21, 2016

WhatsApp-Image-20160712

Msanii Cassim Mganga aka Tajiri wa Mahaba amedai kuumizwa na ukimya wa kundi la Tip Top Connection bila ya kutoa wimbo wowote.

Miaka kadhaa nyuma msanii huyo aliwahi kuwa member wa kundi hilo baada ya kutoka kwenye kundi la La Familia lililokuwa linaongozwa na Chid Benz. Muimbaji huyo amekiambia kipindi Power Jams cha EA Radio kuwa hawezi kujua tatizo la ukimya wa kundi hilo unatokana na kitu gani.
“Unajua unapoongelea Tip Top Connection na Kassim Mganga ni kama familia, hivyo ile ni familia yangu japo tulipishana kwenye masuala ya biashara tu,” amesema Cassim.
“Hivyo kama mwanafamilia wa Tip Top Connection ukimya wao unanigusa na kuniumiza sababu nilikuwa natamani kuona chama linaendelea na moto ule ule kama zamani,” ameongeza.
Kwa sasa msanii huyo ameachia wimbo wake mpya wa taratibu ‘Manuari’ ambao umekuwa tofauti na matarajio ya mashabiki wake.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi