,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Thursday, August 25, 2016

Msanii wa Bongo Fleva Timbulo amesema wimbo wake wa ‘Ngomani’ baada ya kugonga ukuta kwa wasanii wawili wa kike kufanya naye wimbo wake kuanzia msanii Lina na Malaika kutokana na sababu mbalimbali Nay Lee ndiye alikubali bila tatizo.

Akizungumza na EATV Timbulo amesema baada ya ‘managemeni’ yake na Malaika kukubali kuingiza sauti ya wimbo na kushindwa kutokea kwenye video, Timbulo aliamua kufuta sauti ya Malaika katika wimbo huo na kuingiza ya Nay Lee na kufanya naye kazi hiyo.
“Malaika alishindwa kutokea kwenye video kwa sababu vitu alivyokuwa anavitaka ikiwemo mavazi mapya na fedha nilimwambia kazi hiyo tunakwenda kufanyia vijijini hivyo hakuna haja ya mavazi mapya akagoma kutokea ikabidi nimtafute Nay Lee ambaye alikubali bila tatizo lolote” Amesema Timbulo
Aidha Timbulo amesema pamoja na kuachia ngoma hiyo bado anaendelea kuwaomba mashabiki waendelee kumuunga mkono katika kazi zake na ataendelea kufanya vitu vizuri zaidi.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi