,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Monday, August 22, 2016

UCHAGUZI CUF: Wakati uchaguzi mkuu wa CUF ukiendelea Profesa Lipumba alivamia mkutano huo akiwa na wapambe wake wakimtaka kugombea nafasi hiyo. Baada ya mabishano ikaamuliwa wajumbe wapige kura kuamua agombee au kukubali ombi lake la kujiuzulu.

MATOKEO:
-Waliokataa asigombee tena kura 476 sawa na asilimia 97.2%
-Waliokubali agombee kura 14 sawa na asilimia 2.8%.

Pichani ni "Le Profeseri" baada ya "kudondokewa na kitu chenye ncha kali".!

MASWALI 10 KWA PROFESA LIPUMBA.!

By Malisa GJ,

1. Kwanini anataka kurudi kwenye nafasi ya Uenyekiti kienyeji na si kwa kura?

2. Waliochukua fomu ya kugombea Uenyekiti ni watu watatu, yeye hakuchukua. Kama anajiamini kwanini hakuchukua fomu ili agombee nafasi hiyo na kushinda kihalali?

3. Sababu kubwa iliyomfanya Lipumba kujiuzulu ni CUF kama sehemu ya UKAWA kukubali kumpokea Lowassa kujiunga UKAWA kupitia CHADEMA. Lakini Lipumba anataka kurudi wakati Lowassa bado ni mwanaUKAWA na CUF bado ni sehemu ya UKAWA. Sasa nini kinamrudisha, wakati sababu zilizomuondoa bado hazijarekebishwa?

4. Lipumba anadai bado wanachama wa CUF wanamhitaji awe mwenyekiti wao, lakini kwenye uchaguzi wa jana waliokataa asigombee walikua watu 476 sawa na asilimia 97.2%, na waliokubali agombee ni watu 14 sawa na asilimia 2.8%. Je hawa watu 14 ndo wanampa "guts" ya kusema CUF bado inamhitaji?

5. Ikiwa yeye si mjumbe wa mkutano mkuu, kwanini alilazimisha kuingia kwenye mkutano huo kinyume utaratibu tena kwa kupiga walinzi waliokua mlangoni?

6. Kwanini Polisi walimpa ulinzi Lipumba kwenda kuvuruga mkutano wa CUF?

7. Kwanini baada ya vurugu Polisi walitokomea na kuwaacha "vijana wahuni" walioletwa na Lipumba wakipiga watu ukumbini?

8. Lipumba amesahau nini CUF? Mbona analazimisha kutumikia watu wasiomtaka? Nani kamtuma?

9. Ikiwa ameweza kukodi "wahuni" kuja kufanya fujo kwenye mkutano mkuu wa chama chake, je tutakosea tukisema ana nia mbaya na chama chake? Yani lengo lake la kurudi CUF sio ili kuisaidia bali kuhakikisha inaangamia.

10. Lipumba amekuwa Mwenyekiti wa CUF kwa miaka 20 (tangu mwaka 1995 hadi mwaka 2015 alipojiuzulu). Je kuna lipi analotaka kuifanyia CUF sasa hivi ambalo alishindwa kulifanya kwa miaka 20 ya uongozi wake?

NB: Kitendo alichokifanya Lipumba jana kuvuruga mkutano mkuu wa chama chake ni cha aibu na kinamshushia hadhi na heshima yake kwa jamii aliyoijenga kwa muda mrefu. Mwanataaluma wa masuala ya Mahusiano ya Umma (PR) Ndg.Arthur Page aliwahi kusema "unaweza kutumia miaka 20 kujenga hadhi yako ktk jamii (reputation), lakini ukaibomoa kwa sekunde 5". Na hiki ndicho alichokifanya Lipumba. ‪#‎Shame‬.!
 
Malisa G.J - (Facebook)

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi