,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Thursday, August 25, 2016

POLISI Kanda Maalumu ya Dar es Salaam imeanza mazoezi ya ukakamavu katika Mkoa wa Kipolisi wa Temeke kwa lengo la kudhibiti uhalifu.
Akizungumza Dar es Salaam jana baada ya mazoezi hayo, Kamanda wa Kanda hiyo, Kamishna wa Polisi Simon Sirro, alisema mazoezi hayo yatafanyika katika mikoa yote mitatu ya kipolisi.
Mazoezi hayo yalianza saa 1:00 asubuhikatika viwanja vya Polisi Barracks na hatimaye kwenda viwanja vya Mwembeyanga na viwanja vya Zakhem huku askari hao wakiwa na vifaa vyao vya ulinzi. Walipita katika maeneo ya Kongowe na Kigamboni.
“Lengo letu ni kuzuia uhalifu na kupambana na uhalifu hasa ‘panya road’ ambao wamekuwa wakizunguka kwenye maeneo ya Temeke. Mazoezi yetu yamekwenda vizuri na tunaamini wananchi wameona vifaa vyetu vya Jeshi la Polisi na ukakamavu wa askari wetu,” alisema.
Alisema mazoezi hayo hayalengi kuwatisha wananchi ila kuzuia uhalifu wa aina mbalimbali.
Alisema wamekuwa wakifanya mazoezi hayo kipindi cha nyuma lakini sasa ndio wameamua kuwaita wanahabari.
Aidha, alisema mazoezi hayo ni endelevu na baada ya kupita katika Mkoa wa Temeke watahamia Mkoa wa Kipolisi wa Ilala na Kinondoni lengo likiwa ni kukomesha uhalifu katika Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi