,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Wednesday, August 31, 2016

Studio ambayo imeshawahi kufanya hit song mbalimbali ikiwemo ya “Siyo Mchoyo” ya Young D na ngoma kibao, Kiri Records imesemekana kushindwa kulipa kodi ya nyumba ambapo ndipo studio hizo zilipo.
eNewz imeamua kumtafuta muandaaji wa nyimbo kwenye studio hizo, Rash Don, ili kufahamu ukweli wa madai hayo ambapo amesema hajawahi kushindwa kulipa kodi kwenye studio hiyo mbali na yeye kuamua kuihamishia studio hiyo upande wa pili ili kuongeza ukubwa.
Rash Doni
“Sijashindwa kulipia kodi tumeamua kuhamia upande wa pili ili kupanua studio na wasanii wafurahie mazingira ya studio yetu” Alisema Rash Don.
Mbali na madai hayo, Rash Don alizidi kusema kuwa wanahama hapo huku bado kodi waliyo lipa ikiwa haijaisha hivyo bado hawawezi kuwa wana dalili ya kuelekea kudaiwa au kupewa “notice” ya kuhama.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi