,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Monday, August 29, 2016MWANAHALISI - Na Mwandishi wetu - Imechapwa 27 April 2011RIPOTI ya “kikosi kazi” kilichoundwa na mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jakaya Kikwete kutathmini uchaguzi mkuu uliopita, imejaa udanganyifu. MwanaHALISI limegundua kuwa miongoni mwa yaliyodanganywa ni kuhusu umiliki wa mtandao mashuhuri nchini wa Jamii Forum (JF).


Inaelezwa kwamba ripoti ya Mukama inautaja mtandao wa Jamii Forum kuwa unaundwa na vijana kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Lakini uchunguzi wa MwanaHALISI unaonyesha kuwa mtandao huo hauna uhusiano wowote na Chadema.

Kwa mujibu wa nyaraka kutoka Wakala wa Serikali wa Biashara na Leseni (BRELA), JF inamilikiwa na kampuni ya Jamii Media Company Limited iliyosajiliwa 2 Julai 2008 na kupata hati Na. 66333.

Wanahisa wa kampuni hiyo, ni Steven Diallo, mwenye hisa 40, Maxence Melo mwenye hisa 250, Mike Mushi, mwenye hisa 250, Dickson Charles, hisa 40 na Lameck Mussa mwenye hisa 40.
Wanahisa wengine, ni mwandishi wa habari Mbaraka Islam, mwenye hisa 100 na William Malecela, mtoto wa makamu mwenyekiti mstaafu wa CCM, John Malecela, mwenye hisa 40.

Steve Diallo mtoto wa mjumbe wa NEC na mbunge wa zamani wa Ilemela (CCM), Anthony Diallo.

Rais Kikwete aliunda kikosi kazi muda mfupi baada ya kutoa hotuba ya kuadhimisha miaka 34 ya kuzaliwa kwa CCM, mjini Dodoma. Kikosi kilipewa jukumu la kufanya utafiti juu ya mambo ambayo yanaigharimu CCM na ambayo yalisababisha ishindwe kushinda kwa kishindo katika uchaguzi uliopita.Gazeti hili lilipomtafuta William Malecela anayeishi New York, Marekani, kujua iwapo ni mwanachama wa Chadema alisema, “Si kweli hata kidogo.”

Alisema yeye ni mwanachama mwaminifu wa CCM, na kwamba hivi sasa yuko mbioni kufungua tawi la chama hicho mjini New York Marekani. Alisema, “Tatizo la watu wa CCM hawataki kusoma, badala yake wanakuja na ripoti za kuokoteza mitaani. Mimi ni mwanzilishi wa JF, nimekuwa huko tangu kuanzishwa kwake mwaka 2006.”

Kwa upande wake Maxence Melo, anasema wakati mtandao huo unaanzishwa mwaka 2006 kabla ya kampuni kusajiliwa mwaka 2008, kulikuwa na watu wengi sana, wakiwamo vigogo wa CCM.
Anasema mbali na wanachama hao wanaofahamika kwa majina yao, wapo wanachama na viongozi wengi wa CCM, wanaotumia majina bandia.

Naye Islam, mkurugenzi mwingine wa kampuni hiyo amesema, “Hawa watu wameshindwa hata kwenda BRELA kutafuta nyaraka. Hayo yote yaliyosemwa na CCM hayana ukweli hata kidogo. Huo ni uchovu wa kufikiri.”

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi