,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Wednesday, September 7, 2016Kibongo bongo kila msanii hujipima uwezo wake na level gani amesimama kwenye game ya music ifikapo msimu wa Fiesta.Kwasababu msimu huo ndio humuwezesha kila msanii ambaye anafanya vizuri kwa wakati huo kukutana na mashabiki zake na kuweza kujipima ana ushawishi kiasi gani wa kutoa burudani pindi asimamapo kwenye stage.


Ndivyo ilivyo hata kwa rapper Jay Moe ikiwa amepata shavu la kudondosha burudani kwa wana Shinyanga ikiwa ni miaka 7 imepita sasa tangu alipo pata nafasi ya ku-perform kwenye jukwaa la Fiesta kwa mara ya mwisho.
Amesema ilikuwa vizuri kwake pale alipoambiwa amepangwa ku-perform kama msanii wa pili kutoka mwisho katika show hiyo kwani alidai kwamba ilimpa nafasi ya kuwasoma wenzake wanafanya nini ili na yeye aweze kujipanga zaidi na kumfanya kudondosha bonge la show,
Jay Moe alisema kwamba kutokana na muziki ilivyo kwasasa itambidi kuachia ngoma nyingine mwishoni mwa mwezi huu ili kuweza kuendana na ushindani akiwa kwenye stage ukizingatia ni “Pesa ya Madafu” ndio ngoma pekee ambayo inakiki mitaani kwa sasa.
Ni mengi ambayo yameongelewa na mkongwe huyo pale ilipo msogezea mic dakika chache kabla ya kupanda jukwaani kwenye tamasha la Fiesta huko mkoani Shinyanga. Isikilize hapa interview nzima.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi