,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Tuesday, September 27, 2016

Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini Mh. Geum-Young Song amemtembelea Katibu Mkuu Wizara ya mambo ya Katiba na Sheria Prof Sifuni Mchome ofisini kwake jijini Dar es Salaam na kubadilishana mawazo na uzoefu katika sekta ya Sheria nchini na kuona jinsi wanavyoweza kuimarisha ushirikiano baina ya Wizara na Jamhuri ya Korea ili kuiendeleza Sekta ya Sheria nchini.

Akizungumza katika kikao na ugeni huo Prof. Mchome ameelezea kufurahishwa kwake na Jamhuri ya Korea juu ya dhamira yake ya kuisaidia Wizara na Sekta ya Sheria nchini hadi kukubaliana kuwepo na makubaliano kati ya Wizara na nchi hiyo yatakayowezesha Wizara kupata misaada na kujifunza kutoka Korea. Pia amemueleza Mhe. Balozi Song kwamba wizara iko tayari kutekeleza makubaliano watakayokubaliana ili kuimarisha sekta ya sheria nchini na kuishukuru nchi hiyo kwa mpango wake wa kuisaida wizara.
Katibu Mkuu Wizara ya mambo ya Katiba na Sheria Prof Sifuni Mchome  akizunumza na Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini Mh. Geum-Young Song jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kutembelewa na ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo.

  Katibu Mkuu Wizara ya mambo ya Katiba na Sheria Prof Sifuni Mchome  akipokea zawadi kutoka kwa Balozi wa Jamhuri ya Korea nchini Mh. Geum-Young Song.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi