,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Friday, September 30, 2016

Kuna jamaa anajulikana kwa jina la Scorpion anakaa maeneo ya Buguruni huyo jamaa inasemekana ameshafanya matukio mengi sana ya kuwaibia watu na kuwaua huku akiwatoa macho.

Jamaa hilo likatili lisilo na chembe ya huruma amefanya tukio lingine ambapo amempiga visu kaka wa watu na baada ya hapo akamtoa macho yote mawili.

Akielezea kwa uchungu tukio hilo mwanaume aliyefanyiwa tukio hilo mkazi wa tabata Makuburi anasema alikuwa akitokea kazini kwake mida ya saa nne usiku ndipo akashukia maeneo ya buguruni sheli na kwenda katika vibanda vya kuku akawa ananunua ndipo alipotokea jamaa huyo  na kumwambia kuwa anashida aalipomuuliza shida yake jamaa huyo hakujibu chochote na baada ya hapo alianza kumjeruhi kwa kumpiga visu mgongoni na tumboni.


Alijaribu kupiga kelele za kuomba msaada lakini hakuna mtu yoyote aliyesogea kumsaidia japo kulikuwa kumejaa watu wengi barabarani hapo.Hakuishia hapo baada ya kumchoma visu mgongoni na tumboni alimsogeza barabarani kisha akamchoma visu machoni na kumtoa macho huku watu wakishuhudia tukio lote.

Hakutetewa na mtu yoyote kwa sababu watu wanamuogopa ameshafanya matukio mengi kama hayo na mtu anabojaribu kuingilia kibao kinamgeukia.Akiongea na Geha.. Kaka aliyetolewa Macho akielezea kwa uchungu

Mimi nina ofisi yangu iko tabata  nilifunga saa nne nikaona gari zinachelewa ikapita bajaji ikasimama nikapanda ikaenda kuniacha buguruni sheli,Wakati naenda kituoni nikaenda kununua kuku barabarani kwa ajili ya mboga ya nyumbani…

Nikasimama nachagua kuku nikatoa hela kabla hajanirudishia chechi akatokea jamaa huyo mwizi akaniambia “ninashida kaka” nikamwambia “ongea shida yako mana ninaharaka nikitoka hapa nawahi nyumbani” akawa hajasema chochote nikasema huyu mtu kama ni mwizi lakini hapa mbele za watu hatoniibia na mawazo yangu ataniomba hela nitamwambia ale anachotaka nimpe hela niondoke zangu yani hata sijapewa chenchi na muuza kuku nikaanza kupigwa visu vya mgongo wauza kuku wapo hapo hapo watu wako hapohapo hakuna hata mmoja aliyetoa kauli,tena napiga kelele jamani nisaidieni mwizi nikapigwa visu vya tumboni huku anakata nikajaribu nimshike akanin’gata nikapiga sana kelele jamani mwizi ananiua yani wala sisikii kauli zao zaidi ya yule mwizi akisema “yani hapa hakuna mtu atakaye kusaidia”

Baada ya hapo nikapoteza fahamu akanisogeza pembeni akanichoma visu kwenye macho  akaondoka watu wanashuhudia tena nasikia kuna wengine walichukua video,akanivuta barabarani ili nigongwe na gari sasa gari zikawa zinanipisha,kuna watu madereva wa pikipiki walikuwa wanaona,

Yani hapa mimi sioni kitu ambacho naumia sana sasahivi rafiki yangu anakuja naongea nae lakini simuoni mzazi wangu simuoni…

Kuna msamaria mwema alikuja akaniambia anataka kunisaidia nikamwambia anipeleke nyumbani akaniambia hapana wewe umeumia akanipeleka polisi buguruni nikachukua PF3  akanipeleka hospitali Amana ndipo ndugu zangu wakaja wakanipeleka Muhimbili,Nikafanyiwa operation

Anajulikana Buguruni ni mtu wa ajabu sana,

Nilivyotoka Muhimbili nikaenda CCBRT wakaniambia huyu amekutoa macho sikuridhika pia nikaenda KSMC wameniangalia vizuri macho wakanitoa nyuzi wakasafisha wakaniambia wanauwezo wakuniweka macho  bandia lakini uwezo wakuniwekea macho yakafanya kazi hakuna labda nikajaribu India…

Mimi ningekuwa najua buguruni kuna mauaji wala nisingeendaga lakini nilikuwa sijui,sasahivi ukienda kuulizia kuna mtu anaitwa scorpion buguruni utaambiwa huyo muuaji mbaya sana amenitoa macho..

Nimeumia sana dadadangu kwa sababu nina familia nna watoto  kwa mtu yoyote anayenijua mimi lazima aliesana tangu nimeumia walimkataza hata mama yaangu mzazi asije juzi ndio kaja, muda wote analia anakwambia “yani bira wangenitoa mimi lakini sio wewe mwanangu”

Nikikaa huwa nalia sio mara moja kwa siku ninaposikia sauti ya mtoto nalia rafiki yangu alikuwa ananifwata ofisini leo anakuja kuniona nyumbani,nafikiria huyu mtu kwanini kanifanyia hivi wakati kabla hajanitoa macho kila kitu alikuwa ameshachukua…

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi