,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Wednesday, September 21, 2016

Anga la burudani nchini hivi sasa lipo kwenye msisimko wa tenzi ya Wasanii Diamond Platnumz na Raymond ambao wameachia songi la Salome,
ambalo ni marejeo ya songi pendwa lililloimbwa mwaka 2000 na dada yetu wa Kihaya, Saida Karoli, liitwalo ‘Maria Salome’ almaarufu ‘Chambua kama karanga’..
Tumeona uongozi wa WCB chini ya Diamond ukijitoa lawama kwa kuonyesha kuwa kuna makubaliano ya kuurudia huo wimbo baina yao na Dada Saida kupitia menejiment yake.
Sasa hii ni mara ya 3 huu wimbo unatumika kimaslahi. Mara mbili zote zilizopita zilionyesha kama dada hakuambilia kitu licha ya watu wa pembeni kudaiwa kupiga hela ndefu..
Vyombo vya habari vilikuwa vimeshanisahau, leo hii vinanitafuta,” anasikika akisema Saida kwenye kipande cha sauti alichokiweka Diamond Instagram. “Ndugu zangu baadhi wanajua hata sipo duniani, leo hii naona watu mbalimbali wananitafuta, kwakweli nimefunguka, najihisi kuzaliwa upya,” alisema.
Maria Salome ulikuwa wimbo wenye mafanikio makubwa kwa Saida Karoli. Pamoja na kumlipa kwa kuurudia wimbo huo, Diamond amesema asilimia 25 za mapato ya wimbo huo yataenda kwa Saida

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi