,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Wednesday, September 7, 2016

Kiongozi wa Ufilipino Rodrigo Duterte amesema anajutia kwamba amatamshi yake kumhusu kiongozi wa Marekani Barack Obama yamefasiriwa kama matusi.

Bw Duterte amesema hayo baada ya Bw Obama kufuta mkutano wake na kiongozi huyo kutokana na maneno ya lugha chafu yaliyoelekezwa kwake.
Kiongozi huyo wa Ufilipino alikuwa amemweleza Bw Obama kama "mwana wa kahaba" na kuongeza kwamba hatakubali kuulizwa maswali kuhusu ukiukwaji wa haki za kibinadamu nchini mwake.
Alisema Ufilipino haitawaliwi na mtu yeyote. Ufilipino ilikuwa koloni ya Marekani.
Hayo yalijiri kabla ya kufanyika kwa mkutano wa viongozi wa nchi za Kusini Mashariki mwa bara Asia, mjini Laos.
Lakini kupitia taarifa, Bw Duterte amesema anajutia matamshi hayo.
Amesema wanadiplomasia wa Ufilipino na Marekani wanatarajia kuondoa uhasama na tofauti zilizozuka baina ya nchi hizo mbili.
 
Rais Barack Obama alionywa na Bw Duterte "kuonyesha heshima"
Tangu kuingia madarakani, Bw Duterte ameendelea kutumia maneno makali, na kutumia lugha chafu kuwarejelea Papa Francis, maafisa kadha wa Umoja wa Mataifa, waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry na balozi wa Marekani nchini Ufilipino.

Rais wa Marekani Barack Obama amevunja mkutano wake na Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte, ambaye awali alikuwa amemwita "mwana wa kahaba".
Bw Obama awali alikuwa amesema kwamba angemuuliza kiongozi huyo maswali kuhusiana na mauaji ya kiholela ya watu wanaotuhumiwa kuhusika katika ulanguzi wa dawa za kulevya Ufilipino.
Lakini Bw Duterte, ambaye ameunga mkono mauaji hayo, alisema iwapo hilo lingefanyika: "Putang ina (mwana wa kahaba) nitakutusi katika mkutano huo."
Maafisa wa Obama wamesema badala yake kiongozi huyo sasa atakutana na rais wa Korea Kusini.

Msemaji wa baraza la taifa la usalama Marekani Ned Price ameambia wanahabari kwamba Bw Obama atakutana na Bi Park Geun-hye katika mkutano wa Mataifa ya Kusini Mashariki mwa bara Asia (Asean) mjini Laos, ambapo viongozi wamekusanyika kwa mkutano mkuu.

Bw Obama, aliyetua Laos baada ya kuhudhuria mkutano wa G20 mjini Hangzhou, China, alitarajiwa kuuliza maswali kuhusu 

ukiukwaji wa haki za kibinadamu Ufilipino.
Lakini akiongea mjini Manila Jumatatu kabla ya kuondoka kuelekea Laos, Bw Duterte alishutumu hilo na kusema ni "kukosa adabu" na akamtusi rais huyo wa Marekani. Aliongeza kwamba: "Tutagaragazana matopeni kama nguruwe iwapo utafanya hilo."
Kisha, alizungumzia kampeni ya kukabiliana na walanguzi wa dawa za kulevya ambapo washukiwa 2,400, wakijumuisha walanguzi na watumizi, wameuawa nchini Ufilipino tangu achukue mamlaka mwezi Juni.

"Kampeni dhidi ya dawa za kulevya itaendelea. Wengi watafariki, wengi watauawa hadi tuangamize mlanguzi wa mwisho na kumuondoa kutoka barabarani ... hadi mtengenezaji wa mwisho wa dawa hizi auawe, tutaendelea."

Bw Obama awali alidunisha matusi hayo na kusema aliwaomba maafisa wake kuchunguza iwapo huu ni wakati mwafaka wa kuwa na mashauriano ya kufana.
Baadaye, maafisa wake walivunjilia mbali mkutano huo.
Ziara ya mwisho ya Obama bara Asia akiwa kama rais imejaa vioja. Alipowasili Uchina, alijipata kwenye mzozo wa itifaki kati ya maafisa wa Marekani na Uchina ambapo alikosa kuwekewa zulia jekundu.

Matusi

Hii si mara ya kwanza kwa Rais Duterte kutumia lugha chafu kuwarejelea viongozi mashuhuri.
Alimwita Papa Francis "mwana wa kahaba", waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry "mwendawazimu" na majuzi alimweleza balozi wa Marekani nchini Ufilipino kama "mpenzi wa jinsia moja ambaye ni mwana wa kahaba".
Image copyright AP
Image caption Wachanganuzi wanasema tabia ya Duterte inamfanya kupendwa sana nyumbani lakini huenda akatengwa na jamii ya kimataifa
Wachanganuzi wanasema tabia ya Duterte inamfanya kupendwa sana nyumbani lakini huenda akatengwa na jamii ya kimataifa.
Umoja wa Mataifa tayari umeshutumu ukiukwaji wa haki za kibinadamu nchini humo.

Mwezi Agosti, wataalamu wawili wa haki za binadamu kutoka Umoja wa Mataifa walisema agizo la Bw Duterte kwa polisi na umma kuwaua washukiwa wa ulanguzi wa dawa za kulevya ni "uchochezi wa ghasia na mauaji, na ni uhalifu chini ya sheria za kimataifa."

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi