,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Tuesday, September 27, 2016

 
José Mário dos Santos Mourinho Félix, GOIH, known as José Mourinho, is a Portuguese professional football manager and former football player. He is the manager of Premier League club Manchester United. 
Born: January 26, 1963 (age 53), Setúbal, Portugal
Height: 5′ 9″
Full name: José Mário dos Santos Mourinho Félix
Spouse: Matilde Faria (m. 1989)
Teams coached: Manchester United F.C. (Manager, since 2016), 

 Posted  Jumanne,Septemba27  2016  saa 12:31 PM

Kwa ufupi;-

Kila mtu anatetea kibarua chake, hivyo Mreno huyo amegundua kwamba kuendelea kukumbatia matatizo yatamgharimu zaidi katika kazi yake ya kuinoa Manchester United, hivyo amekunjua makucha kwa kuwapiga chini mastaa wote anaodhani ni shida na anafanya hivyo bila ya kutazama sura ya mtu.

J
OSE Mourinho hataki ujinga kabisa kwenye kazi yake. Kibarua chake kimetikisika na kuona hivyo akatazama nani ni tatizo, akaibuka na uamuzi mmoja wa kumpiga chini nahodha wake Wayne Rooney.

Kila mtu anatetea kibarua chake, hivyo Mreno huyo amegundua kwamba kuendelea kukumbatia matatizo yatamgharimu zaidi katika kazi yake ya kuinoa Manchester United, hivyo amekunjua makucha kwa kuwapiga chini mastaa wote anaodhani ni shida na anafanya hivyo bila ya kutazama sura ya mtu.

Kwanza ameanza na nguli wa klabu hiyo, Rooney na panga litampitia pia kiungo Mbelgiji Marouane Fellaini, watasubiri sana benchi. Mourinho amempiga marufuku Rooney kuzungumzia viwango vya wenzake wakati yeye mwenyewe yupo hovyo zaidi, huku Fellaini ambaye alikuwa na zali la kuanzishwa mechi zote za mwanzoni akicheza sambamba na Paul Pogba kwenye kiungo, zamu ya kusugua benchi imemfikia rasmi baada ya kocha huyo kudai kwamba, ameona Pogba anaelewana zaidi na Ander Herrera.
“Pogba kucheza vizuri? Hakucheza vibaya dhidi ya Southampton. Hakucheza vibaya pia dhidi ya Hull City. Ipo hivi, timu inapocheza vizuri, naye anakuwa mzuri zaidi. Tunatarajia mengi kutoka kwake, lakini nimeona Pogba na Herrera wanaelewana zaidi, pacha wa uwanjani.”

Kuhusu Rooney, Mourinho anaripotiwa kuketi kitako na staa huyo na kisha kumweleza kwamba, kitu ambacho anatakiwa kufanya kwa sasa ni kuhangaika kupandisha ubora wa kiwango chake na si kuendelea kuwahubiria wachezaji wenzake kucheza vizuri wakati tatizo kubwa linaanzia kwake. Rooney anaripotiwa kutumia muda mwingi vyumbani kuwasema wenzake kuhusu viwango vyao wakati timu hiyo ilipochapwa 2-1 na Manchester City, wakati mwenyewe alikuwa hovyo kwenye mechi hiyo na mechi nyingine zilizofuatia kabla ya kupiga benchi dhidi ya Leicester City Jumamosi iliyopita.
Ripoti zimefichua kwamba Rooney mwenyewe amekubaliana na ukweli kuhusu kiwango chake na anatambua itakuwa ngumu kupata nafasi katika kikosi cha kwanza, lakini hawezi kufikiria kuondoka kwenye timu hiyo hadi mkataba wake utakapofika tamati ambapo kwa sasa umebakiza miaka miwili.

Gwiji la Man United, Gary Neville, ambaye aliwahi kucheza na Rooney kwenye klabu hiyo na kwenye timu ya taifa ya England kabla ya kuwa kocha, alisema fowadi huyo itabidi akubaliane tu na hali halisi ya kuchezeshwa kwa awamu na Mourinho.
“Hiki ni kipindi cha mpito katika maisha yake ya soka, kipindi ambacho umuhimu wake utakuwa katika mtazamo tofauti,” alisema Neville.

Wakati Rooney na Fellaini ikionekana kubana upande wao, kuna wachezaji wanne wanaonekana kuwa na nafasi kubwa na kupewa nafasi zaidi katika kikosi cha kwanza ambao ni Juan Mata, Marcus Rashford, Jesse Lingard na Zlatan Ibrahimovic. Hizi sura zitaonekana sana kwenye timu ya Mourinho. Imefichuka kwamba Rooney atarudi kikosi kwenye mechi ya Europa League dhidi ya Zorya Luhansk, lakini atarudi benchi kwenye Ligi Kuu England dhidi ya Stoke City Jumapili.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi