,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Saturday, September 17, 2016

In radio studio
Kituo cha redio, Magic FM cha Dar es Salaam kimetii agizo la TCRA la kuwataka wamuombe radhi Rais John Magufuli.

Amri hiyo ilitolewa na Joseph Mapunda,Makamu mwenyekiti wa kamati ya maudhui ya TCRA, kutaka kituo hicho cha redio hiyo kuomba radhi kwa Rais Magufuli na watanzania kwa ujumla baada ya kukiuka kanuni za utangazaji na kumkashifu Rais na kuchochea uvunjifu wa amani.
“Sisi kama uongozi tumeridhishwa na maamuzi ya kamati ya maudhui kuhusiana na tatizo ambalo tumelipata katika kipindi cha ‘Morning Magic,” amesema Mkurugenzi wa vipindi wa kituo hicho, Dativius Mango.
“Imekuwa ni sehemu moja ya kujifunza na changamoto, lakini kubwa ni kwamba kwa adhabu ambayo tumepewa kwamba tumuombe radhi mheshimiwa Rais John Magufuli, tutafanya hivyo katika habari zetu, habari ya saa kumi kamili jioni, saa tatu usiku. Lakini changamoto nyingine ni kukaa karibu na watangazaji wetu ili tuweze kuhakikisha basi jambo kama hili lisiweze kujirudia,” alisisitiza Mango.
Katika adhabu nyingine, kituo cha Radio 5 kimefungiwa kwa miezi mitatu.
BY: EMMY MWAIPOPO

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi