,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Tuesday, September 20, 2016

*SEMINA YA NENO LA MUNGU*
*MWALIMU*: C MWAKASEGE


*SOMO*:_MAMBO YA KUFANYA ILI FIKRA ZAKO ZITUMIKE KUFANIKISHA MAISHA YAKO_
*UKUMBI*: VIWANJA VYA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM
*TAREHE*: 18th SEPTEMBER 2016

*Lengo la Somo:*
_Kutambua maarifa ya kutumia fikra zako kupata Mafanikio maishani._

*MSINGI WA SOMO.*
Mithari 23:7a
*_Maana aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo._*

NB; Neno Fikra na Fikira ni neno moja kwenye Biblia. Usipate shida ukiona yameandikwa tofauti.
*Fikra*-
 

Kwanza,ni mkusanyiko na mtiririko wa mawazo unaotengeneza msimamo wa kiutekelezaji ndani ya mtu.
Kwahiyo fikra sio tu tunavyowaza au kufikiri. Ni zaidi ya hapo.Ni matokeo ya jinsi uonavyo kwa namna na jinsi ulivyo. Au jinsi uonavyo. Au unavyotafakari nafsini mwako.

Pili,fikra inaonyesha ulivyo kimaisha. Inaonyesha kiwango chako cha kufikiri kilipo au kilipofika.

Tatu,fikra ziliumbwa zikae ndani ya nafsi ili zitumike kuweka aina na kiwango cha maisha ya mtu katika kila eneo linalomhusu. Unaposoma Biblia utagundua MTU ni ROHO inayokaa ndani ya 

MWILI. Lea Chujagi

Kazi ya nafsi ni kiungo kati ya Roho na Mwili ili kuwasiliana baina yao. Roho na Mwili haviendani lugha zao. Ndipo nafsi ikawepo kuleta mawasiliano. Nafsi huunganisha ulimwengu wa kiroho na wa kimwili. Ndani ya nafsi ndiko kwenye fikra. Nafsi ina akili. Mwili una ubongo.

*3 Yohana 1:2*
 

Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo.
Tofauti ya aina ya viwango vya maisha haina ya MTU na MTU inatokana na namna wanavyofikiri. Hajalishi mpoje,namna zenu za maisha zinategemea tofauti zenu za kufikiri.

*2 Wakorintho 11:3*
 

Lakini nachelea; kama yule nyoka alivyomdanganya Hawa kwa hila yake, asije akawaharibu fikira zenu, mkauacha unyofu na usafi kwa Kristo. _Shetani akitaka kuharibu maisha yako ya kiroho huanza kwenye nafsi. Kwenye fikra. Fikra ni mpango mkubwa sana. Kama alivyowaharibu Adamu na Eva pale bustanini Eden. Hata MTU akitaka kuokoka vita huwa kwenye fikra. Mungu wa ulimwengu huu hushambulia fikra._

*_HATUA ZA KUFUATA ILI KUTUMIA FIKRA ULIZONAZO ZIKUSOGEZE VIWANGO ALIVYOKUSUDIA MUNGU._*
1. _TATHMINI NI MAISHA YAKO ILI UJUE KIWANGO CHAKO CHA KUFIKIRI KWAKO KILIVYO_

*Hii haijalishi upo kwenye hali gani. Hii itakusaida kujua unaanzia wapi ili kushughulikia na kufikiri kwako. Unajua ni kwanini unaweza kwenda kwenye chuo ukapewa mtihani tena ingawa ulifaulu? Huwa wanachek fikra. Hata kusaidiwa huja baada ya kujua fikra zako. Shule inapaswa ikupe MAARIFA SIO ELIMU*
Biblia iliweka MAARIFA ili uweze kufanikiwa. Mfano kwenye kina Daniel walipotakiwa kuwekwa ili kutumika na mfalme walipimwa maarifa sio elimu zao.

*Kwahiyo unapoenda mbele za Bwana kwanza ni lazima ujitathmini. Vigezo vya kujitathmini ndivyo hufanya uweze kujitathmini. Mfano,kuwa mzima unatembea barabarani sio kigezo cha kwamba u mzima. Kapime kwanza vipimo ndio utajua kweli. Kwenye mambo ya kiroho inakuwa shida sana. Kwa wakristo vigezo ni Agano letu ndani ya Kristo Yesu. Vigezo hivi ni vikubwa. Sana*

*2 Wafalme 4:1-7*
 

_Basi, mwanamke mmoja miongoni mwa wake za wana wa manabii alimlilia Elisha, akasema, Mtumishi wako mume wangu amekufa; nawe unajua ya kuwa mtumishi wako alikuwa mcha Bwana; na aliyemwia amekuja ili ajitwalie wana wangu wawili kuwa watumwa.2 Elisha akamwambia, Nikufanyie nini? Niambie; una kitu gani nyumbani? Akasema, Mimi mjakazi wako sina kitu nyumbani, ila chupa ya mafuta.3 Akasema, Nenda, ukatake vyombo huko nje kwa jirani zako wote, vyombo vitupu; wala usitake vichache.4 Kisha uingie ndani, ukajifungie mlango wewe na wanao, ukavimiminie mafuta vyombo vile vyote; navyo vilivyojaa ukavitenge.5 Basi akamwacha, akajifungia mlango yeye na wanawe; hao wakamletea vile vyombo, na yeye akamimina.6 Ikawa, vilipokwisha kujaa vile vyombo, akamwambia mwanawe, Niletee tena chombo. Akamwambia, Hakuna tena chombo. Mafuta yakakoma.7 Ndipo akaja akamwambia yule mtu wa Mungu. Naye akasema, Enenda ukayauze mafuta haya, uilipe deni yako; nayo yaliyosalia uyatumie wewe na watoto wako._

*Vitu ambavyo utaviona kwa mwanamke huyu mfiwa ni.....*

i. Fikra zake za kimaisha mama huyu mjane zilikwamia mahali zilipokwamia fikra za mume wake. Maadamu mume alikuwa hai na Mke aliegemea anapoishi mumewe. Mume alipokufa mke hakujua la kufanya. Hakuwa na namna za kuendeleza fikra za mumewe mbele zaidi. Alikwenda kwa Elisha kwakuwa hakuwa na cha kufanya.Kufa kwa mumewe kuliua sehemu ya maisha ya yule mama. Ukiolewa sio kwamba akili yako isifanye kazi. Mnapaswa kuungalisha fikra zenu. Ndio mana mali za wengi hupotea mume akifariki.

ii. Hali ya maisha na kiwango cha maisha cha mama huyu kilitokana na ulipofika mtiririko na mkusanyiko wa fikra za mume wake. Ukiangalia maisha ya baba yule angalia maisha ya familia yake. Mtiririko wa fikra za mume ndio ulileta kiwango cha maisha ya familia ile. Angalia wengi wakiacha kazi. Maisha yao husimama. Kwakuwa wengi huwa na fikra za kampuni sio zao.

iii. Fikra za mume wake zilitengeneza viwango vya maisha yake na ya familia yake kutoka kwenye maeneo yafuatayo.

a. Utumishi aliokuwa nao kwa Elisha. Haitajwi allowance wala chochote alikuwa akipata lkn familia ilikuwa inafaidika kwa namna flani

b. Kumcha Bwana pia ilikuwa kigezo kingine. Maisha yakawa ya naenda.

c. Alikuwa anaishi kwa mkopo. Mama anakiri kuwa walikuwa wanakopa na mume amekufa kabla ya kulipa. Hii maana yake muulize mumeo anatoa wapi hela kabla hujaanza kudaiwa. Huyu mama walichukua mpaka watoto. Biblia haikatai mikopo lkn inakataa riba.

Huyu baba alikuwa ni mcha Mungu lkn alikuwa na maisha ya shida. Kama uchaji wako haujacharge fikra zako hutaenda kokote hapa duniani ingawa utaenda mbinguni. Tukitaka kujua fikra zako tunaangalia maisha yako.

d. Mume wa mjane alimjengea Mke wake kufikiri kuwa maisha yao yalitokana na ushauri na muongozo wa Elisha na kumbe sivyo. Ndio mana mama alipofiwa tu na mume moja kwa moja alienda kwa Elisha. Kwanini huoni kwenye Biblia mama huyu akienda kwa mmoja wa ndugu wala marafiki? Anaenda kwa Elisha.

*Elisha hakumwambia kuwa atamkopesha. Au atamuajiri. Akampa maagizo mengine.*

e. Mama mjane hakujua cha kufanya juu ya fikra za mume wake kuwa kawaweka watoto wao rehani. Yani hakuandaliwa na mazingira hayo. Hakujipanga. Aliona kama mumewe ataishi milele. Mume alikopa yeye lkn aliweka rehani watoto. Kwa namna hii alikuwa anawawekea watoto wake fikra za KITUMWA.
Biblia haisemi yule baba alipokuwa anapata pesa alikuwa anapeleka wapi? Lkn tunawaona watoto wanawekwa rehani. Watoto wakikua watafikiria deni aliloacha baba yao. Na huu ni utumwa. Masharti ya mikopo huwa yanakufunga fikra za kufikiri. Unakuwa unawazia deni tu. Huu ni utumwa. Ni fikra za kitumwa.

f. Fikra zake na za mume wake hazikuwa na uwezo wa kutumia walichokuwa nacho ili kuwatengenezea maisha mazuri. Mama anapojibu kuwa sina kitu inaonyesha namna alivyokuwa anafikiri. Hakuitaja kwanza chupa ya mafuta. Hakuiwazia hiyo. Fikra zake zilikuwa haziwazii chupa ya mafuta. Alikuwa na watoto ambao walishiriki kubeba chupa za mafuta. Walitaka kupelekwa utumwani,maana yake walikuwa na uwezo wa kufanya kazi nyingine kuleta kipato nyumbani. Sio kufa njaa.

*Unaweza ukawa na kipawa au cheti au chochote lkn huna fikra za kujitoa kwenye hali uliyonayo.. Tatizo ni fikra. Fikra ni pesa. Fikra ni kila kitu. Biblia inasema tutumie akili lkn tusitegemee akili zetu.*

_Home Work!_
 

1. Chanzo cha mapato yako kinatoka wapi?
2. Na je kikifika mwisho au kufa utafanyaje?
3. Fikra zako zinahusika kwa kiwango gani katika upatikanaji wa mapato yako
*Mungu ametuita kuishi kwa NENO na sio MUUJIZA.*
Ooh halleluja!

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi