,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Saturday, September 17, 2016

Meneja wa Diamond Platnumz na WCB Salam amefunguka na kuweka wazi sababu za wao kwenda nyumbani kwa Rais Jakaya Kikwete na kusema kuwa walikwenda kuwatambulisha wasanii wao wapya ambao wapo chini ya 'Label' ya WCB Wasafi.

Akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio Salam alidai kuwa wakati Mh. Jakaya Kikwete anaondoka maradakani, Diamond Platnumz alikuwa bado hajatambulisha wasanii wengine chini ya label hiyo walikwenda kuwatambulisha kwa Jakaya Kikwete wasanii kama Raymond, Rich Mavoko na kukabidhi kazi zao.
"Unajua wakati Mh Jakaya Kikwete anatoka madarakani Diamond Platnumz bado alikuwa hajasaini wasanii wengine chini la WCB Wasafi, hivyo tulikwenda kuwatambulisha kina Harmonize, Raymond pamoja na Rich Mavoko pia na kukabidhi kazi zao, lakini uzuri wakati tunakabidhi kazi Mh Jakaya Kikwete alikuwa amevutiwa na wimbo wa Harmonize wa matatizo, akawa anasema alikuwa kwenye gari aliisikiliza kazi hiyo na kusema kuwa kijana ameimba sana. Hivyo kwetu sisi ilitupa moyo sana tunashukuru Mungu tulibadilishana naye mawazo mawili matatu na kuomba chochote kinachoweza kupatikana au nyezo zozote zinazoweza kusaidia muziki wetu wa Tanzania kufika mbele zaidi ndicho tulichoomba kwani yeye ana mtandao mkubwa wa watu kuliko sisi" alisema Salam

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi