,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Monday, September 12, 2016

Msanii wa bongo fleva,Baraka Da Prince kupitia akaunti yake ya instagram ameweka ujumbe unaoashiria amekua kifikra na kiakili na yuko tayari kuendelea mbele zaidi.

Katika ujumbe huo,Baraka amewashukuru wote waliomspati toka mwanzo na kuwaomba msamaha wote aliwaowakosea pia kuwataka mashabiki zake kukaa tayari kwa kitu kikubwa kutoka kwake ambapo inasadikikwa kuwa ni kolabo yake na Ali Kiba.
Kupitia Instagram yake aliandika” It’s almost a year tangu nilipoachia kazi yangu ya mwisho, Siwezi. Katika kipindi hiki nimepitia mambo mengi sana. Nimekuwa kiakili, kifikra na kisanaa na sasa nipo tayari kuianza safari mpya.
Kufika hapa leo haikuwa kazi rahisi, pamoja na kipaji changu nilichojaaliwa na Muumba, lakini labda bila usaidizi mkubwa niliopata kutoka kwa baadhi ya watu, pengine nisingekuwa hapa leo, hivyo ningependa kuwashukuru wazazi wangu na familia yangu, #TetemeshaRecords #RoyalNsyepa ,Media zote, Radio & TV Personalities, Waandishi wa habari na msingi mkuu wa sanaa yangu – mashabiki wa muziki wangu. Asanteni sana kwa support yenu na kama kuna yoyote niliwahi kumkosea naomba #Nisamehe – kukosea kwangu ndio ukamilifu wangu kama mwanaadamu
Leo hii September 10, 2016, natangaza kuianza safari mpya kimuziki kwenda kuiteka Africa na dunia, naomba mnisupport kijana wenu???????????????? *(Follow me Twitter @barakatheprince for a MAJOR ANNOUNCEMENT) #IamARockstar #CrownPrince@rockstar4000 “.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi