,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Saturday, September 24, 2016

Msanii Juma Nature ameelezea kusikitishwa kwake na tukio lilitokea kwa msanii mwenzake KR Mullah ambaye alikuwa naye kwenye kundi moja la Wanaume Halisi, na kisha kwenda Radr Entertainment.

Akizungumza kwenye kipindi cha FNL cha East Africa Television na East Africa Radio, Juma Nature amesema alipotumiwa picha za KR Mullah akiwa amelewa chakali huku hajitambui, alihuzunika sana kwa msanii huyo kufikia hatua hiyo.
"Mimi roho iliniuma sana, na ilinikuta nipo nyumbani, hata namba zangu sijui walipata wapi wale majaa, kwa sababu mimi mwenyewe sio mtu wa kutoka usiku", alisema Juma Nture.
Juma Nature aliendelea kusema kuwa KR Mullah ana haki ya kwenda popote na kufanya kazi, kwani hayo ndio maisha ya wasanii na hana tatizo na hilo.
"Mullah ni mwanaume, yani ukisikia Wanaume Halisi ndio kina KR Mullah, ye kuondoka kwake kwenda kwingine ni sawa, ndio maisha yetu wasanii, lakini KR Mullah sio wa kumuamini tena, unaweza ukamlipa mpaka hela na asije kwenye show", alisema Juma Nature.
KR Mullah alikuwa ni miongoni mwa wasisi wa kundi la Wanaume Halisi, lakini kwa sasa yupo kwenye uongozi wa Radar Entertainment ya TID, kitu mabcho wengi wanakilaumu na kusema msanii huyo ataingizwa kwenye makundi mabaya ya matumizi ya madawa yakulevya, kutokana na watu anaojihusisha nao kuwa na kashfa hizo.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi