,./.,

,,

... ...

';';';';

,.,.

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

\\..\\

Thursday, September 22, 2016

 
 UBUYU wa town unamuhusu mkali wa Ngoma ya One More Night na zao kutoka Jumba la Kuibua Vipaji (THT), Khadija Said Maige ‘Kadja Nito’ ambaye anadaiwa kuwa mbioni kubadili dini sambamba na kufunga ndoa na mchumba wake wa muda mrefu anayejulikana kwa jina moja la Lisimo.


 Kwa mujibu wa chanzo cha uhakika ambacho ni rafiki na staa huyo aliyewahi kubamba na Ngoma ya Maumivu, wawili hao walikutana eneo la mazoezi ambalo
linamilikiwa na mchumba wake huyo. “Kadja alikuwa akienda kwa Lisimo ambaye anamiliki eneo la mazoezi huko Kinyerezi, taratibu wakaanzisha uhusiano. Siku nyingine wanaonekana pamoja maeneo anayoishi huko Kinondoni na sasa jamaa yupo siriazi kuishi naye jumla kama mke na mume,” kilisema chanzo.
 Chanzo kinaendelea kumwaga ubuyu kuwa, kutokana na Kadja kuwa Muislam na jamaa huyo Mkristo, hivyo wamekubaliana ambapo Kadja atabadili dini na kuolewa. “Kwa sasa Kadja yupo katika mipango ya kubadili dini japo wazazi wake kama wanataka kumuwekea kauzibe hivi, lakini ndiyo kwanza hasikii wala haambiwi na ndoa ya Kikristo lazima ifungwe,” kiliweka nukta chanzo. Baada ya kushibishwa ubuyu huo, Showbiz Xtra lilianza kumsaka Lisimo ambaye simu yake iliita bila kupokelewa lakini lilipomnyanyulia Kadja waya na kumsomea madai hayo, alifunguka bila kupepesa; “Yote unayosema ni kweli, nipo mbioni kuolewa ila hilo la wazazi kunimaindi kisa nataka kubadili dini hayo ni mambo ya kifamilia sababu familia yangu ni watu wenye maadili ya Kiislam ila naamini kila kitu kitaenda sawa. Kifupi tu, natarajiwa kuolewa mwishoni mwa mwezi wa kumi,” alisema Kadja

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi