,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Wednesday, September 21, 2016

saida-karoli

Kusahaulika kwenye muziki wa Tanzania ni rahisi kama kumsukuma mlevi hata kama uliwahi kutoa nyimbo zilizohit kila kona.

Saida Karoli ni mmoja wa wahanga. Amekiri kuwa kabla ya Diamond kuurudia wimbo wake, Salome, vyombo vya habari vilikuwa vimemtupa kulee – vichache tu vilivyokuwa vinakumbuka hata kama yupo hai, kwa mujibu wa maelezo yake.
“Vyombo vya habari vilikuwa vimeshanisahau, leo hii vinanitafuta,” anasikika akisema Saida kwenye kipande cha sauti alichokiweka Diamond Instagram. “Ndugu zangu baadhi wanajua hata sipo duniani, leo hii naona watu mbalimbali wananitafuta, kwakweli nimefunguka, najihisi kuzaliwa upya,” alisema.
Maria Salome ulikuwa wimbo wenye mafanikio makubwa kwa Saida Karoli. Pamoja na kumlipa kwa kuurudia wimbo huo, Diamond amesema asilimia 25 za mapato ya wimbo huo yataenda kwa Saida.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi