,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Saturday, September 10, 2016

14233083_1186466538063429_1472346303529214408_n
Aliyekuwa mtangazaji wa kipindi cha Clouds 360 cha Clouds TV, Hudson Kamoga amekuwa ni mmoja kati ya wakurugenzi 11 walioteuliwa na Rais wa John Magufuli Jumamosi hii.
Aidha, Rais amemteua Eliya Ntandu kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa nafasi ya Katibu Tawala Mkoa wa Songwe ilikuwa wazi na uteuzi huu umeanza leo.
Imeeleza kuwa Ntandu pamoja na Makatibu Tawala walioteuliwa jana ambao ni Ado Mapunda aliyeteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara na Tixon Nzunda aliyeteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa wataapishwa katika tarehe itakayotangazwa baadaye.
Rais Magufuli amefanya uteuzi wa Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya 11, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji mmoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa moja ili kujaza nafasi zilizokuwa wazi katika Halmashauri hizo.
Wakurugenzi walioteuliwa ni kama ifuatavyo Godwin Kunambi(Manispaa ya Dodoma), Elias Ntiruhungwa(Mji wa Tarime), Mwantumu Dau( Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba), Frank Bahati(Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe), Hudson Kamoga(Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu), Mwailwa Pangani(Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo).
Wengine ni Godfrey Sanga(Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama), Yusuf Semuguruka(Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga), Bakari Mohamed(Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea), Juma Mnwele(Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo), Butamo Ndalahwa(Halmashauri ya Wilaya ya Moshi), Waziri Mourice( Halmashauri ya Wilaya ya Karatu) na Fatma Latu( Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo)

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi