,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Friday, September 30, 2016

 Displaying 14520430_1373110129380724_6421501612043637888_n.jpgMultichoice yakabidhi vifaa maalum vya michezo kwa watu wasioona ambavyo vitawawezesha kuhudhuria maadhimisho ya siku ya kimataifa ya fimbo nyeupe tarehe 06/10/2016 itakayofanyika mkoani Mbeya. Lengo kuu la maadhimisho hayo ni kuhamasisha jamii na watumiaji wa barabara, kuiheshimu fimbo nyeupe, na  kumsaidia asiyeona anapotembea na anapohotaka kuvuka barabara.

Vifaa vilivyotolewa ni: Mipira (4) ya goalball, 
Displaying 14449891_1373109996047404_551063183049063713_n.jpgDomino set nne,Karata nne, fedha za nauli na kujikimu kwa timu hiyo ya wasioona. Mchango huo wa Multichoice unathamani ya jumla ya shilingi 3,120,000/=. Akitoa msaada huo mkurugenzi mkuu wa Multichoice Tanzania Maharage Chande alisema “Multichoice inafuraha kubwa kushirikiana na nduguzetu wasioona wa Dar es salaam katika kuwaandaa kushiriki maadhimisho yatakayofanyika Mbeya, kama kampuni ya kitanzania tutaendelea kuwa mstari wa mbele kushirikiana na jamii yetu kila fursa inapojitokeza”.
Kampuni ya MultiChoice Tanzania inaomgoza kwa kutoa burudani za michezo na filamu kwa kupitia DSTV. Makao makuu yake ni Dar es salaam na Inamatawi Mwanza, Arusha, na Mbeya. 

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi