,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Wednesday, September 14, 2016

Image result for dada wa bilionea msuya

UPANDE wa Jamhuri leo umetoa majibu ya hoja ya kutaka kufutiwa mashtaka ya mauaji inayomkabili mke wa marehemu bilionea Erasto Msuya, Miriam Mrita na mfanyabiashara Revocatus Muyela.

Awali, wakili wa washtakiwa, Peter Kibatala aliwasilisha maombi ya wateja wake katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa kile alichodai kuwa hati ya mashtaka ilikuwa ina mapungufu kwa kuwa haioneshi kama washitakiwa hao walikuwa wana nia ovu.

Mtuhumiwa Miriam Mrita akiwa na askari magereza kuelekea chumba cha kusikiliza kesi inayomkabili.
Akijibu hoja hiyo ya Kibatala mahakamani hapo, wakili wa serikali, Diana Lukundo alisema hoja zote walizoziwasilisha na upande wa washtakiwa haziko kisheria na kuna aina mbalimbali za kuwasilisha mashtaka.
Baada ya upande huo wa Jamhuri kujibu hoja hizo za upande wa washtakiwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkazi Mkuu, Magreth Bankika, mahakama hiyo inatarajia kutoa maamuzi ya hoja hiyo Septemba 27, mwaka huu.


Mtuhumiwa, Revocatus Muyela baada ya kutoka mahakamani.
Awali ilidaiwa mahakamani hapo kuwa, mnamo Mei 25, mwaka huu maeneo ya Kibada Kigamboni jijini Dar es Salaam, Miriam Mrita na Revocatus Muyela, walimuua kwa kumchinja dada wa bilionea Msuya, Anathe Msuya.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi