,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Monday, September 19, 2016

Taasisi ya Mikono Speakers International imetangaza kuchangia 10% ya mapato yake kutoka kwenye Kongamano kubwa inayolitayarisha "FINANCIAL SERVICES EXPO 2016" linalotazamiwa kufanyika Mwezi November Mwaka huu katika Hoteli ya Kilimanjaro Mjini Dar. Akizungumza na Waandishi mbali mbali wa Habari nchini leo katika Hoteli ya Hiloday Inn Mjini Dar, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Ndugu Deogratius Kilawe amesema Asilimia hiyo Kumi ni sawa na karibu Shilingi za Tanzania Millioni 20. Kilawe alisema wamesikitishwa sana na Maafa makubwa yaliyoletwa na Tetemeko la Ardhi lililowakumba wananchi wa Mkoa wa Kagera na wanaungana na Serikali katika mpango wake wa dharura wa kuwasaidia wananchi wa Kagera.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mikono Speakers International Bw. Deogratius Kilawe akizungumza na Waandishi wa Habari leo katika Hoteli ya Holiday Inn, pia wengine aliofuatana nao ni Meneja wa Masoko wa Taasisi hiyo Rozzy Dossa na Mkurugenzi wa Masoko pia wa Taasisi hiyo Niss Richard, kwenye mkutano huo Bw. Kilawe alitangaza rasmi azma ya Taasisi hiyo kuchangia mfuko wa dharura wa maafa ya Tetemeko la Ardhi Kagera.
0 comments:

Post a Comment

ufunguzi