Kampuni ya Samsung imesitisha utengenezaji wa simu za Galaxy Note 7 baada ya hofu kuendelea kuwepo kuwa hata zile simu za mara ya pili zilizodaiwa kurekebishwa zinaweza kulipuka.
maxresdefault
Mtu anayefahamu uamuzi huo kwa ukaribu, amethibitisha kupitia CNN usitishwaji wa muda wa simu hizo baada ya shirika la habari la Korea Kusini,
Yonhap kuripoti kwanza kuhusiana na taarifa hizo.
Tangazo hilo limekuja baada ya makampuni ya Marekani na Australia kusema yataacha kufidia simu hizo kwa walionunua mwanzo kutokana na wasiwasi kuwa simu hizo nazo ni vimeo kama za awali.

Mapema baada ya Galaxy Note 7 kuingia sokoni mwezi August, baadhi ya watumiaji walidai kuwa simu zao zilikuwa zikishika moto. Kampuni hiyo ililazimika kuziondoa sokoni simu zote kwa kudai zina tatizo la betri linalopeleka zichemke na hivyo kuwaka moto.
Simu mbadala zilikuwa zimalize tatizo hilo na tayari baadhi ya watumiaji walipewa zingine. Lakini baadhi ya wateja bado wamekuwa wakiripoti kuwepo kwa tatizo hilo hatari kwenye simu zao mpya.