,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Wednesday, October 19, 2016

Jumatano ya October 19 Ligi Kuu soka Tanzania bara iliendelea kama kawaida kwa michez0 mitano kuchezwa huku mchezo wa sita wa Azam vs Mtibwa Sugar ukitarajiwa kuchezwa usiku wa leo katika uwanja wa Azam Complex Mbande Chamazi.
Kwa upande wa Mabingwa watetezi klabu ya Dar es Salaam Young Africans ilirudi kanda ya ziwa kucheza dhidi ya Toto Africans huku ikiwa na kumbukumbu ya kufungwa goli 1-0 na Stand United siku kadhaa nyuma katika uwanja wa Kambarage Shinyanga, hiyo ilikuwa ni baada ya kuvuna point tatu dhidi ya Mwadui FC.
Yanga wamerudi kanda ya ziwa safari hii kucheza dhidi ya Toto Africans na wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 2-0, magoli ambayo yalifungwa na mzambia Obrey Chirwa dakika ya 28 na goli la pili lilifungwa na Simon Msuva dakika ya 55 kwa mkwaju wa penati, Obrey Chirwa leo anakuwa kafunga goli lake la pili akiwa na Yanga.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi