,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Thursday, October 13, 2016

Image result for multichoice tanzaniaMultichoice Tanzania imedhamini wateja wake 6 walioshiriki kwenye mashindano redioni. Washindi hao wataenda kuhudhuria tamasha la mziki la MAMA’s, litakalofanyika mjini Johannesburg Afrika Kusini  mnamo tarehe 22, Oktoba, 2016. Tamasha hilo maarufu la mziki linafanyika kila mwaka, na DStv ni kingamuzi pekee kitakachorusha hewani shindano hilo maarufu la mziki kupitia chaneli yake ya mziki ya MTV-base 322, saa 4 usiku, mubashara. 

Tanzania kwa mashindano ya mwaka huu inawakilishwa na Navykenzo, Diamond, Alikiba & Sauti Sol, Yamoto band, Vanessa Mdee na Rayvan . Ambao ni wasanii walioteuliwa kuwania tuzo hizo. Watanzania wanahimizwa kuwaunga mkono wasanii wetu kwa kuwapigia kura kwenye mitandao ya kijamii kama Facebook, Twitter na Instagram, na tovuti ya http://mama.mtv.com/voting/. Huduma ya  DStv itatuwezesha kutazama tamasha hilo la mziki huku tukiwashangilia wasanii wetu.
Mkurugenzi mtendaji Maharage Chande, alisisitizia umuhimu wa kuwaunga mkono washiriki wetu kupitia huduma ya DStv premium, ili kuweza kubudurika na tamasha hilo la mziki. Hoja hii iliungwa mkono na wasanii waliohudhuria mkutano huo wa vyombo vya habari kwenye ofisi za Multichoice.

MKURUGENZI MTENDAJI WA MULTICHOICE TANZANIA NA WASHINDI WA TUZO ZA  AMVCA 2016, WAHIMIZA WATANZANIA KUSHIRIKI KWENYE MASHINDANO YA AMVCA YA 2017.
Mkurugenzi mtendaji wa Multichoice Tanzania  akiongelea mashindano ya Africa Magic Viewer’s  Choice Award (AMVCA) kwenye mkutano na waandishi wa habari alisema “ Africa Magic Viewers Choice Awards ni tuzo maarufu barani Afrika, zenye lengo la kutambua na kusheherekea kazi na mchango mkubwa unaotolewa na watengeneza sinema, wacheza sinema na mafundi mitambo katika tasnia ya filamu na televisheni. Washindi wa tuzo hizi wanaheshimika Afrika nzima na kuzawadiwa taji la ushindi katika hafla kubwa inayofanyika kila mwaka. Kwa mwaka huu, hafla hiyo itafanyika  Machi 3-4, 2016.”
Mr. Maharage Chande aliendelea kusema “Tanzania tuna sababu kubwa ya kushiriki na kuamini kwamba tuna uwezo wa kushinda tuzo hizo. Kwani mwaka huu tulikuwa na washindi wawili, single Mtambalike kupitia filamu yake ya “Kitendawili” iliyokuwa filamu bora ya lugha ya Kiswahili, na Elizabeth Michael kupitia filamu yake ya “Mapenzi” iliyoshinda filamu bora ya Afrika Mashariki.
Tumejaribu, tumeweza, sasa tujaribu tena mwaka huu kwa kuwasilisha filamu zetu ambazo tunaona zina uwezo wa kushinda. Kushiriki ingia kwenye tovuti ya http://www.amvca2017.com, tarehe ya mwisho ya kuwasilisha filamu zetu ili zishindanishwe ni tarehe 28, Oktoba 2016.
Mashindano haya hushindanisha wasanii kwenye maeneo 27, miongoni mwa maeneo hayo ni wacheza filamu, mafundi wa mitambo, na filamu zenyewe,  filamu nzuri ya Kiswahili, wahariri wa picha, na wahandisi wa sauti za filamu. Katika hafla hiyo, msanii Single Mtambalike alihimiza watanzania wenzake kutosita kushiriki kwenye mashindano hayo kwa kutuma kazi zao ili kuitangaza na kuiendeleza vizuri sanaa ya Tanzania.

Multichoice Tanzania kupitia huduma zake maarufu za DStv, imekuwa katika mstari wa mbele kuiburudisha  jamii kwa vipindi tofauti. DStv ilirusha hewani tamasha la Africa Magic Viewers Choice Awards ya Machi 5, 2016 iliyoandaliwa na Multichoice Africa. 

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi