,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Monday, October 31, 2016

Rais Magufuli aliyeko ziarani nchini Kenya amelazimika kutembea kwa miguu kufuatia msongamano mkubwa wa magari kwa kile kilichodaiwa barabara haikuwa imeandaliwa kwa kiongozi huyo kupita.

Mashuhuda wa tukio hilo waliimbia tovuti ya The Star ya nchini Kenya kuwa Rais Magufuli alitembea kwa sababu ya msongamano wa magari katika barabara kuu ya Uhuru alipokuwa akielekea lilipo kaburi la Rais wa Kwanza wa Kenya, Mzee Jomo Kenyatta.
6
Watumiaji wengi wa mitandao nchini Kenya wameandika kuhusu kitendo hicho cha ujasiri cha Rais Magufuli huku wakiwaponda viongozi wao kuwa hawana ujasiri huo.

Rais Magufuli amewasili nchini Kenya kwa ziara ya siku mbili kufuatia mualiko wa Rais Uhuru Kenyatta ambapo pamoja na mambo mengi anatakayoyafanya, atatembelea kaburi la Rais Jomo Kenyatta, atazindua barabara jijini Nairobi na kujadiliana na Rais Kenyatta kuhusu mambo mengi ikiwa ni pamoja na ada wanayotozwa wanafunzi wa Kenya Tanzania, masuala ya kibiashara na diplomasia.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi