,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Thursday, October 6, 2016

Taarifa ya awali ya tukio la kupigwa mwanafunzi wa Mbeya Day ndg Sebastian Chingulu.


Tukio lilianza tarehe 26/9/2016 mwalimu Frank Msigwa mwanafunzi kwa vitendo toka chuo kikuu cha Dar Es salaam kutoa assignment ya soma la kingereza kwa wanafunzi wa kidate cha Tatu.

Baada ya kusahihisha aligundua kuwa kuna baadhi ya wanafunzi hawakufanya NA tarehe 28/9/2016 alikwenda darasani NA kutoa adhabu NA alianza kwa kuwapa adhabu ya push up, kupiga magoti NA baadae viboko 2 katika utekelezaji mwanafunzi Sebastian Chingulu alikataa kufanya kutokana NA kuumwa NA goti.

Baada ya kukataa adhabu mwl Frank Msigwa NA wenzake 2 John Deo NA sanke Gwamaka walimpeleka ofisini NA kuanza kumshambulia kwa kipigo NA baada ya tukio hilo walitoeka na wakati wanamshambulia mwalimu mwingine aliwasihi wasimpige NA alirekodi tukio hilo.

Serikali ya mkoa inaendelea kuwashikilia walimu NA mwalimu mkuu kwa mahojiano, kupata maelezo ya wanafunzi waliopata adhabu NA mwanafunzi aliyepigwa.

Nawahakikishia serikali itawasaka popote walipo walimu hawa waliofanya tukio hili NA kufikishwa ktk vyombo vya dola NA sheria.

Aidha mwanafunzi aliyepigwa anaendelea kupimwa NA matibabu.

Hii Ni taarifa ya awali nitaendelea kutoa taarifa kwa kila hatua.


Amos G Makalla
RC Mbeya


 
Waziri wa Elimu Prof. Joyce Ndalichako amewafukuza chuo Waalimu waliokuwa katika mafunzo kwa vitendo Shule ya Mbeya Sekondari kwa kumpiga kikatili Mwanafunzi.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi