,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

,.,.

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Thursday, October 6, 2016

3Alivyokuwa mdogo alikataa kusoma mama yake mzazi alishafariki siku nyingi na alikuwa akilelewa na mama yake mdogo maeneo ya Yombo buza.
Alishawahi kufungwa jela japo haijajulikana alikosa nini, na jina lake kamili ni Salum Njwope na jina hilo nila babu yake. Yeye ni mwenyeji wa mkoa wa Shinyanga. 
Kwa mujibu wa mama yake mdogo anasema Scorpio alipokua akitoka nyumbani usiku saa mbili anamuaga mama yake mdogo huyo kuwa anakwenda kwenye kazi ya ubaunsa katika club kumbe mwenzie alikuwa anaenda Buguruni kuibia watu mpaka asubuhi ndio anarudi nyumbani.
Pia scorpion ashawahi kushiriki katika shindano lililojulikana kama Dume Challenge kama miaka mitatu iliyopita na aliibuka mshindi. Napia alianza mafunzo ya kucheza caret tangu akiwa mdogo sana napia ni mtu mwenye nguvu za kuzaliwa nazo.
Kuna kipindi aliondoka nyumbani kwao kwa muda mrefu mama yake mdogo anadai alikuwa hajui yuko wapi mpaka baadae aliporudi mwenyewe nyumbani.
Amekamatwa na Polisi baada ya kutuhumiwa kumjeruhi mkazi mmoja wa Dar es Salaam eneo la Buguruni kwa kumng’oa macho katika kitendo kilichoelezwa kuwa ni wizi wa fedha.
 
whatsapp-image-2016-10-06-at-11-36-14-am whatsapp-image-2016-10-06-at-11-36-14-am-1 whatsapp-image-2016-10-06-at-11-36-16-am whatsapp-image-2016-10-06-at-12-45-07-pm


Mkazi  wa Machimbo Yombo jijini Dar es Salaam, Salum Njwele (34) maarufu kama Scorpion, amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala kujibu mashitaka ya unyang’anyi wa kutumia silaha na kumtoboa macho yote mawili Said Mrisho.

Scorpion alifikishwa mahakamani hapo jana mbele ya Hakimu Mkazi, Adelf Sachore na kusomewa mashitaka na Wakili wa Serikali, Munde Kalombola.

Akisoma mashitaka hayo, Kalombola alidai kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo Septemba 6, mwaka huu eneo la Buguruni Sheli wilaya ya Ilala.

Munde alidai, Njwele aliiba mkufu rangi ya fedha wenye uzito wa gramu 34 ikiwa na thamani ya Sh 60,000, bangili na fedha taslimu Sh 331,000 vyote kwa pamoja vikiwa na thamani ya Sh 476,000 mali ya Mrisho.

Kalombola alidai kuwa mshitakiwa kabla na baada ya wizi huo, alimchoma kisu machoni, tumboni na mabegani mlalamikaji ili ajipatie mali hizo.

Hata hivyo, upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na upande wa mashitaka uliomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutaja.

Hakimu Sachore aliahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 19, mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena. Mshitakiwa alirudishwa rumande kutokana na mashitaka yanayomkabili kutokuwa na dhamana.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi