,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Sunday, October 9, 2016

Diamond Platnumz amesema katika label yake ya WCB, yeye huchangia vitu vidogo sana na kwamba management yake chini ya Babutale na Mkubwa Fella ndiyo wanaowaangalia wasanii na kuona kama wasanii hao wana vipaji na uvumilivu.
Akiongea na East Africa Radio kwenye kipindi cha Planet Bongo, Diamond Platnumz alisema:

“Kiukweli wasanii wanaokuja kwenye label yangu mimi huwa si mchunguzi sana, lakini management yangu ndiyo huwa inaangalia wakina bosi Tale na Mkubwa Fella wao ndiyo wanaangalia huyu msanii ana kipaji au hana. Wao ndiyo wanajua huyu mambo iko huku au hamna. Wao wanaangalia vitu vingi wanaangalia kama msanii ni mvumilivu. Hivyo kuna vitu vingi wao wanakuwa wanaangalia kutokana na uzoefu wao katika muziki na kudeal na wasanii. Kuna wasanii wanaweza kula msoto mpaka unawaonea huruma, lakini ndiyo hivyo ukitaka kuingilia tu watakuwambia ‘hapana usiingilie tuache kuna jambo tunalitazama.”

Staa huyo aliongeza na kusema yeye mchango wake huwa ni mdogo kwa mfano katika hatua za mwisho kuona msanii yupi anastahili kutoka kwa wakati upi, au kama msanii ana mapungufu fulani yeye anaweza kuchangia mawazo labda msanii huyo afanye kitu gani ili mwisho wa siku aweze kutoka.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi