,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

,.,.

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Friday, October 7, 2016

      MWALIMU  Wiseman Ficky KUTOKA  CHUO  KIKUU  CHA DAR ES  SALAAM..
    
Chini  ujumbe  wake  kupitia  mtandao  wa facebook
Leo mada kubwa iyo break internet ni tukio la walimu wakioneka wanatoa adhabu kubwa sana kwa mwanafunzi.
Tukio hilo limepekea kila mtu ni lawama kwa walimu, walimu leo tumepokea matusi ya kila aina.
Nisema wazi mimi ni mwalimu kitaaluma. Ni mwalimu hasa wa kusomea nilishapita shule na kufundisha miaka kadhaa kabla sijaamua kurudi zangu tena chuoni ninaposoma hivi sasa.
 
Nikiri kwamba kitendo walichofanya hawa si chema, ni kitendo kibaya lakini tunapolamu basi tuwe na staha. Tusifanye hii taaluma kuwa chochoro kila mtu anapaswa kuisemea. Hebu mheshimu taaluma za watu. Nalaani vikali mkiotukana walimu humu mitandaoni kuita walimu vilaza, washenzi, mashetani waliofeli, nk Haiingii akilini kosa la walimu wawili watatu likufanye kutukana walimu wote Tanzania.
 
Walimu ni watumishi na binadamu pia wanakosea wao si malaika, kama ambavyo polisi hukosea kupiga raia, daktari hukosea kwa wagonjwa, trafiki nao hukosea kudai rushwa, watumishi wengine mbali mbali hukosea basi na hawa walimu nao wamekosea na wamefanya makosa lakini hatupaswi kutukana walimu nchi nzima.
 
Narudia tena acheni matusi ya reja reja shenzi kabisa nyie kwanza mnapata wa ujasiri wa kuwatukana walimu ambao hata wewe umepita mikononi mwao?!
Je hakuona walimu wenye busara, wenye upendo waliojitolea kwa moyo wote kukufundisha mpaka ukajua kusoma na kuandika na ngazi zote za elimu hadi ukafika ahpo ulipo?!
 
Waliokufundisha unawaita vilaza waliofeli? Mnazungumzia kufeli kupi? Hivi kuna mwalimu div zero? Yani unashupaza kabisa shingo eti hakuna mwalimu division one au division 2? Hebu njoo Leo Udsm faculty of education ukikosa div one in two 1500+ njoo uropoke tena humu mtandaoni.
 
Niwapongeze wote walioamua kuangalia hili hili jambo kwa busara na kulaumu kwa busara bila kutukana walimu wao.
Taaluma ya elimu ya elimu nchini ina changamoto nyingi sana. Walimu wa sasa wanakumbana na changamoto nyingi sana kuanzia katika mazingira yao ya kazi hadi kwa wawanafunzi wanaowafundisha ieleweke sasa hivi jaami iko hovyo kimaadili jambo linalopelekea baadhi ya watoto kuwa na nidhamu mbovu.
 
Leo nipo serious kabisa.
Wapo vijana wamefikia hadi kupiga walimu wao, kuwatukana matusi ya nguoni. Imetokea wanafunzi kupiga mwalimu na kumtoa meno huko katavi cha ajabu sijaona reaction kama ya leo huku mitandaoni.
 
Tufahamu kwamba shule nyingi serikali mwanafunzi hafukuzwi hata Mkuu wa Shule hana uwezo wa kumfukuza mwanafunzi kwa maana ya kumtoa kabisa shuleni jambo hilo limepeleka baadhi kutumia hiyo kama kigezo wanajua wazi hawawezi kufukuzwa watakupiga itajadiliwa na itaisha.
Hebu leo hii wewe vaa viatu vya mwalimu aliepigwa mtama na mwanafunzi wake mstarini, vaa viatu vya mwalimu alietolewa meno huko katavi. Vaa viatu vya mwalimu anaeambiwa na mwanafunzi wake darasani hunibabaishi na hunitishi wewe ni mjinga tu bila shaka ingekua ni wewe unayelamu humu mitandaoni pengine ungefanya makubwa kuliko hata walimu wa kwenye ile clip
Wapo wanafunzi ni wala bangi wazuri sana wao siku moja shule siku moja road kuendesha boda boda. Ni manunda haswaa sasa walimu wamekua chaka la walama baada ya jamii kuishindwa kuiweka sawa mitoto yenu huko nyumbani mnaisukumia Shule walimu wahangaike nayo na ndio hii inayopiga walimu na kuwakaba makoo kisa tu ameulizwa kwa nini hujaandika class work.
 
Walimu hawa vijana wako field bado hawajawa walimu kamili wapo masomoni pengine mwaka wa kwwnza hawajamaliza bado kozi ya ualimu walikua hawana uzoefu na changamoto za watoto minunda na ndio hizo wamekutana nazo na kupelekea kushindwa kudhibiti hasira zao.
 
Walimu wakiwa bado jikoni hawajaiva wanapelekwa field wakakumbane na mazingira halisi ya shule ili kuwajengea uwezo kamili sasa mbaya zaidi mambo yamekua kama haya.
 


Wasalaam
 


Mwalimu kijana Wiseman Ficky
Imeandikwa na Wiseman Ficky

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi