,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Friday, October 21, 2016

Ni wiki chache tu zimepita tangu tuanze kuziona cheche za mwanadada Linah katika kurasa zake za mitandao ya kijamii kuhusu mahusiano yake mapya.Kama ilivyo Shilawadu sio watu wa mchezo mchezo wamezinyaka za ndani za mpenzi huyo mpya wa mwanadada Linah. inasemekana kwamba jamaa huyo ni mchumba wa mtu na amekwisha pata mtoto mmoja na huyo mchumba wake, na walikuwa katika hatua za mwisho za kukamilisha taratibu za ndoa kabla ya mwanadada Linah kumpora kidume huyo.Zilinyakwa na Gossip Cop Soudy Brown, ndipo akaamua kumvutia waya mwanadada Linah na kupiga nae story kuhusiana na hilo.
Linah amekanusha vikali kuwa mpenzi wake ni mchumba wa mtu bali akadai kuwa anachokifahamu yeye ni kwamba amekwisha zaa tu na msichana huyo ambaye wanadai ni mchumba wake lakini mahusiano yalikwisha vunjika kitambo.
Amewatolea mapovu sio ya polepole wanaosambaza habari hizo na kuwaambia kuwa yeye ni mke mtarajiwa wa bwana Shabani na muda sio mrefu mambo yatajipa.
Sitaki nikuchoshe, wacha nikupe nafasi ya kuisikiliza hapa U-Heard ya leo October 19 umsikie mwanadadaLinah anavyo funguka kuhusu mpenzi wake huyo mpya. Itazame hapa chini.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi