,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Tuesday, October 4, 2016

Image result for MAMA DIAMOND VS ZARIIJUMAA ya wiki iliyopita haikuwa njema kwa Sanura Kassim ‘Sandra’, mama wa staa wa Muziki wa Kizazi Kipya anayefanya poa kwenye gemu, Nasibu Abdul ‘Diamond’ baada ya kusambaa ujumbe kwenye mitandao ya kijamii, unaodaiwa kuwa ulinaswa kutoka kwenye simu yake akimtumia shoga yake ambaye hajafahamika jina, ukimhusu Zarinah Hassan ‘Zari’ aliyezaa na Diamond.
UJUMBE ULIKUWAJE? Katika ujumbe uliokuwa unasambaa, picha ya message ‘screen shot’ ya meseji iliyodaiwa kutoka kwa mama Diamond, ilikuwa ikionesha kwamba mwanamke huyo alikuwa akiomba msaada kwa shoga yake wa kumsaidia ‘kumchamba’ Zari mitandaoni na kama ikiwezekana, waende kumroga ili aachane na Diamond.

Image result for MAMA DIAMOND VS ZARI VS WEMA

TEAM ZARI WATOKWA POVU 
Baada ya kunaswa kwa ujumbe huo, kundi linalomsapoti Zari kwenye mitandao ‘Team Zari’ lilianza kumshambulia mama Diamond kwa kumshushia mitusi ya nguoni na kumtuhumu kwamba eti yeye ndiye amekuwa chanzo cha mwanaye kutodumu na wanawake kwenye mapenzi kwa sababu anamuingilia na kumgombanisha nao. 

Image result for MAMA DIAMOND VS ZARI

MAMA DIAMOND AJA JUU 
Baada ya kusikilizia ‘machafuko’ yaliyokuwa yakiendelea kwenye mitandao ya kijamii, hasa Instagram, mwandishi wetu alimtafuta mama Diamond na kutaka kujiridhisha kama ujumbe uliokuwa ukisambaa mitandaoni ni kweli ulitoka kwake na sababu zilizomfanya aandike maneno hayo. Baada ya kumpata na kuzungumza naye, mama Diamond alikuja juu na kueleza kuwa ‘hapendagi ujinga’ linapokuja suala la mambo ya kifamilia, akakanusha kwamba ujumbe huo haukuwa umetoka kwake na kwamba ulitengenezwa na wabaya wake kwa lengo la kumchafulia sifa mbele ya jamii.
 “Kwanza sipendagi ujinga mimi! Hata ukiangalia DP (display picture- picha ya utambulisho wa mtumiaji wa Instagram) haifanani na ninayotumia kwenye akaunti yangu halisi. Kwanza mimi ni mtu mzima na akili zangu, siwezi kutuma meseji kama hiyo, siwezi kuweka mambo ya kifamilia kwenye mitandao wala kwenye vyombo vya habari.
“Natukanwa sana mitandaoni hasa baada ya bethidei yangu na zaidi matusi yameongezeka baada ya mimi kum-wish hepi bethidei Wema (Sepetu- ex wa mwanaye) lakini sina muda wa kubishana nao, Mungu atawalipia,” alisema mama Diamond. Mwandishi wetu alipomuuliza ni hatua gani anafikiria kuwachukulia watu waliofanya mchezo huo, alisema awali alifikiria kwenda polisi lakini busara zikamtuma kuacha kwani akilipeleka suala hilo mbele ya sheria, watakaokamatwa ni wengi kwa sababu anatukanwa na wengi na haoni sababu ya kufanya hivyo.

2 comments:

  1. kumpa mtu keki kwa mkono wa kushoto maana yake nini?kwanini wengine wapewe nawa kulia?utasema ni mapenzi yako!!kwanini hujamtakia heri ya kuzaliwa mkweo zari?utasema ni hiari yako,yamkini hata simba pia hukumtakia!wote wanao,kama mama mtu mzima ulivyosema tumia utu uzima wako ili haya yasikukute!Mungu anakuona hivyo!Shukuru Mungu mwanao anapendwa na jamii,hivyo hata jamii inakuchukulia wewe kama mama yao,chochote utakachokifanya kikaonekana tofauti utajikuta unakumbana na wanaokereka na mambo hayo!nanyinyi mliokuwa wapenzi wa simba,leo hamko nae kampenda alienae huko nyumbani kwa mama simba mnatafuta nini?kwanini msiende kwenu?au kwa wapenzi mlionao?nanyinyi pia ni chanzo cha mama sima kushambuliwa!kaleni keki zenu kwenu!acheni unafiki na uswahili!mlipewa nafasi hamkuzitumia sasa mnakuwa vivuruge wa familia za watu,acheni,kaeni nao mbali!mjue kuna wenu wanawasuburi,tafakarini mlipokosea ili mkijapata mtulie tuli!kila siku nyi nyi tu! loh, pepo gani hilo?

    ReplyDelete
  2. This family is just disastrous to their son's career.No matter how much he defends them they are out right evil and its very clear! God bless u Zari if possible leave these swahili people alone u are strong u can take care of your family.

    ReplyDelete

ufunguzi