,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Tuesday, October 4, 2016

Meneja wa PPF Kanda ya Temeke Mama Erica Sendegeya akiwakabidhi baadhi ya  wanachama wapya 395 waliojiunga na PPF huko Ikwiriri katika wilaya ya Rufiji mkoa wa Pwani leo mchana.

PPF YAKABIDHI KADI ZA WOTE SCHEME KWA WANACHAMA WAPYA 395 WA IKWIRIRI MKOANI PWANI

NA MWANDISHI WETU, IKWIRIRI
MFUKO wa Pensheni wa PPF, kupitia mpango wa Uchangiaji wa Hiari, “Wote Scheme”, umesajili zaidi ya wanachama 395  huko Ikwiriri wilayani Rufiji mkoa wa Pwani.
Akizungumza hivi karibuni na waandishi wa habari wakati wa zoezi la  ugawaji wa kadi za uanachama wa PPF  kwa wajasiliamali wa Ikwiriri kwenye viwanja vya Chuo cha Maendeleo, Meneja wa PPF Kanda ya Temeke, Erica Sendegeya, alisema,  wanakijiji hao wajasiriamali walihamasika kujiunga na mpango huo baada ya Kanda Temeke kutoa elimu juu ya umuhimu wa wananchi kujiunga na Mfuko huo kwani kuna manufaa  mengi.
“Tuliwaeleza, mpango huu wa Wote Scheme umebuniwa ili kutoa fursa ya wananchi walioajiriwa kama mfumo wa ziada au waliojiajiri wenyewe, wakiwemo wakulima, wavuvi, wafugaji, Boda boda  na mama lishe, kujiunga na Mfuko kwa kuchangia kima cha chini cha shilingi 20, 000 kila mwezi. “Fedha hizo unaweza kuzitoa kwa mkupuo au kwa awamu kulingana na uwezo wa mwanachama,” alifafanua Sendegeya.
Akielezea faida za kuwa mwanachama, Meneja huyo alisema, “Mwanachama atafaidika na Huduma ya Afya kupitia NHIF.” Alisema na kuongeza kuwa faida nyingine ni pamoja na mwanachama kujipatia mkopo wa maendeleo ya biashara kwa  masharti nafuu, mkopo wa elimu, pamoja na fao la uzeeni, alisema Meneja huyo.
Kuhusu namna mwanachama anavyoweza kuchangia baada ya kujiunga na Mpango huo, Meneja Uhusiano wa PPF, Lulu Mengele alisema, “Mfumo huo una njia rahisi ya kuwasilisha michango yake, ambayo ni kwa kutumia simu za mikononi ambapo huduma hii imemrahisishia mjasiriamali kuchangia michango yake popote alipo” Alisema.
Baadhi ya wanakijiji waliojiunga na Mpango huo, wameipongeza PPF kwa kutoa elimu ambayo imewafanya wajiunge na Mfuko huo na ni matarajio yao utasaidia kuboresha shughuli zao.
“Mimi ni mfuga nyuki, kilichonivutia ni jinsi Mfuko huu unavyoweza kutoa mikopo ya maendeleo” alisema Erasto Joseph, ambaye pia ni mjasiriamali.
Naye Ishara Ibrahim ambaye ni mkulima, alisema, ni matarajio yake kuwa kujiunga na PPF, basi ataweza kumudu kupata huduma ya afya kupitia Bima ya Afya.” Alisema.0 comments:

Post a Comment

ufunguzi