,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Monday, October 3, 2016

Majengo yaliyojengwa yatumiwe na shuleYA msingi Simike na sekondari itajengwa palipokuwa shule YA msingi simike
Ni mgogoro na mvutano wa muda miaka 4 kati ya watalaam wa Jiji na madiwani Asema GN namba 157 na Waraka namba 9 hairuhusu kujenga sekondari NDANI YA eneo la shule YA msingi
- wananchi wafurahishwa na uamuzi huo wasema hicho ndicho walichokusudia awali , wawalaumu wanasiasa
MKUU wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla amesitisha mpango wa kujenga sekondari YA kata YA Mabatini NDANI ya eneo la shuke YA msingi mabatini eneo ambalo ni dogo sana 
Uamuzi huo ameutoa leo alipotembelea ujenzi wa majengo hayo na kuongea na wazazi , baraza la maendeleo la Kata ,viongozi wa mitaa sita na jiji 
Wananchi wamemweleza Mkuu wa mkoa kusikitishwa na maamuzi YA wanasiasa hususani madiwani kubadili mawazo YA awali ambapo wananchi walichangia na kujenga majengo hayo kwa lengo la kuhamisha shule ya msingi simike ihamie shule YA msingi Mabatini na Shule hizo mbili zitenganishwe na ukuta na majengo YA shule ya msingi simike yakarabatiwe na mengine kujengewa mapya ili kuwa sekondari lakini cha kusikitisha wanasiasa wamegeuza mpango huo na kutaka majengo mapya shule ya msingi mabatini yawe YA sekondari
Kufuatia mvutano huo mkuu wa Mkoa amefika na kuamuru mpango wa awali ubaki kama ulivyo majengo mapya yatatumiwa na Shule YA msingi Simike na majengo YA simike yatakarabatiwa na mengine kujengwa mapya kwa ajili ya sekondari YA Kata 
Amefikia maamuzi hayo kwa kuzingatia tangazo la serikali namba 157 na waraka wa elimu na 9 vyote vinakataza kujenga sekondari ndani YA shule ya msingi na pia imeweka masharti YA ukubwa wa eneo kuwa shule ya msingi itajengwa kwenye eneo la ukubwa ekari 1.5-4 lakini eneo la shule ya msingi mabatini linalotaka kujengwa sekondari ni ekari 1.37
Kwa msingi huo amesitisha mpango huo na kuelekeza Mkuu wa wilaya, mkurugenzi jiji, watalaam na madiwani kusimamia ukamilishaji wa shule ya msingi Simike na baadaye sekondari

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi