,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Friday, October 28, 2016

DAR ES SALAAM: Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda leo ametoa siku 14 kwa Wakuu wa Wilaya za Jiji hili kuhakikisha machinga wote wanafanyia biashara katika maeneo waliyopangiwa.
“Kauli ya Rais aliyoitoa kwamba machinga wasibugudhiwi isitumike vibaya kwani hata wao hawapaswi kuwabugudhi wananchi wengine kwa kufanya biashara zao mbele ya maduka na barabarani,”amesema Makonda.
Ameongeza kuwa anatambua kuwa machinga wanajitafutia riziki lakini hawapaswi kuvunja sheria kwa kufanya biashara hata katika maeneo yasiyokuwa rasmi.
“Barabara zimejengwa kwa gharama kubwa hivyo haziwezi kubadilishiwa matumizi na kuwa sehemu ya machinga kupanga na kuuzia bidhaa zao” amesema.

Na Hilaly Daud/Gpl

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi