,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Friday, October 21, 2016

Msanii anayefanya poa kwenye mziki wa Hip Hop kutoka Arusha, pia anafanya vizuri kwa sasa na ngoma zake pamoja na Cover alizofanya, Motra the Future, kashangazwa na kitendo cha P-funk kuachia kazi yake.

Kinachoonekana Motra the future hakujua kabisa kuwa wimbo wake ft baraka Da price upo mtandaoni na mtu yeyote anaweza kuusikiliza katika website ya Bbc.
majani187-20161015-0001
Project ya Motra the future aliyofanya kwa P-funk huenda ilitegemewa kutoka kwa style ya kipekee hasa kutokana na tetesi za motra kumkimbia producer wake Mona Gangstar na kukimbilia kwa P-funk jambo ambalo baadaye walilikanusha.
Kupitia Planet Bongo ya EA radio, Motra aliulizwa endapo ana taarifa hizo akashtuka na kuhoji kwanini P-funk ameamua kuutoa wimbo huo wote bila kumshirikisha?
Motra amesema alikuwa akijipanga kwenda kuuchukua ili kuuachia rasmi lakini hakujua tayari upo mtandaoni.
Wimbo huo unasikika kwenye site ya Bbc katika makala maalumu kuhusu muziki wa Bongo fleva iliyoandaliwa na mtangazaji wa shirika hilo Salim Kikeke.
Katika makala hayo kwa lugha ya kiingereza P-funk anasikika akielezea jinsi ya kutengeneza Beat na mwisho wimbo wa Motra ft baraka unasikika wote.
Taarifa za uhakika zinaeleza tayari motra ameshaondoka kwa monagangstar na ana management mpya itayosimamia kazi zake.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi