,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Thursday, October 13, 2016

Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

New Kuna msemo kuwa "ukiona mwenzio ananyolewa wewe anza kutia maji"... unaweza kusema msemo huu unaendana na ushauri wa kuwa nyumba ya jirani ikianza kuungua ya kwako anza kuhamisha vitu. Tumeshuhudia mgogoro mkubwa umetokea chama cha CUF kufuatia maamuzi yao ya huko nyuma kuhusiana na UKAWA na baadaye kumkaribisha Lowassa ndani;


Naamini kabisa kuwa sababu hizo hizo zitakapoiva ndani ya CHADEMA zitasababisha mgogoro mkubwa na wa kihistoria ndani ya chama hicho. Mgogoro huo naamini utasafisha na kuunda mwelekeo mpya wa vyama vya upinzani nchini na inawezekana yakatokea mapokezano (transfer) ya uongozi kutoka kizazi kilichovuruga upinzani kwenda kwa kizazi cha wapinzani wa kweli.

Mabadilishano haya ya kizazi (generational exchange) yatakuwa na matokeo makubwa sana kwa baadhi ya wanasiasa ambao majina yao yamekuwa yakitajwa kila upinzani unapotajwa. Hata hivyo, mgogoro mkubwa zaidi utatokea CHADEMA kama ulivyotokea CUF na NCCR-Mageuzi. Pamoja na hayo naamini kati ya vyama vyote hivi CHADEMA itaweza kusalimika kama chama kipya cha upinzani baada ya kizazi kipya kusahihisha makosa ya watangulizi wake.

Tutaona wanasiasa wetu mashuhuri wakichagua upande tena... swali kubwa ni nani atakuwa upande gani? Nani atakuwa tayari kumsaliti fulani? Nani atakuwa tayari kwenda kinyume na yule aliyesimama naye kabla..

It will be legendary... epic in one word.

Nani anabisha?

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi