,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Friday, October 28, 2016

Mwanamume mmoja nchini Marekani, ambaye ameanza kufahamika kama “binadamu mti”, alikamatwa baada kuvuka barabara akiwa amevalia majani na matawi ya mti na kuingia mtaani.
Asher Woodworth, kutoka Jimbo la Maine nchini Marekani, alijifunika kwa matawi na kuvuka barabara polepole.
Alikuwa amepakia picha yenye vazi jingine linalokaribiana na hilo kwenye mtandao wa Tumblr mwezi uliopita

Polisi walimsindikiza hadi kando mwa barabara kabla ya kumuweka kizuizini.

Asher ambaye ni mwigizaji mjini Portland, Maine baadaye aliachiliwa huru na polisi.

Alisema kuwa alikuwa akivuka barabara mara ya tatu pale alipokabiliwa na maafisa wa polisi.

Asher Woodworth pia aliweka picha hii ukurasa wake wa Tumblr

Anasema: “Nilipata wazo hili nilipokuwa natafakari sana siku moja.”

Anasema alikuwa anataka tu kuwashangaza watu kwa mavazi yake na kuwafanya “watafakari upya kuhusu matarajio yao”.

Alikuwa ametumia matawi ya miti ya aina mbalimbali na anasema ilimchukua yeye na rafiki yake saa kadha kukamilisha vazi hilo.

Anasema matawi ya miti aliyokuwa amevalia yalikuwa “yananukia”.

Lakini mbona akaamua kuvalia matawi ya miti?

“Huwa nahisi nina uhusiano wa karibu na miti, naipenda sana,” aliambia.

Alikuwa pia ametiwa moyo na mpiga picha Charles Freger, aliyepiga picha hii iliyo hapa chini.

Baada yake kukamatwa, Asher Woodworth anasema alikaa saa sita kizuizini kabla ya kuachiliwa huru Jumatatu.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi