,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Tuesday, October 4, 2016

14448452_521934251338996_6433858230564159488_n
Mtoto akikinyea kiganja cha mamaye, haimaanishi kuwa mama atakikata. Atachukua maji na sabuni na kukiosha, na maisha yataendelea – mapenzi tele!

Ndicho hicho ambacho TID amekifanya kwa mwanae kimuziki, Bill Nas. Baada ya kuwepo kwa kipindi cha muda mrefu cha vuta nikuvute kati yao kwenye vyombo vya habari, wawili hao wameonesha kulizika shoka la mapambano yao ya maneno na kuyaacha yaliyopita yapite.
TID amepost picha na video akiwa na hitmaker huyo wa Pozi Chafu, akimkaribisha kwa moyo mmoja Unyamani.
“Wassup, I am with my boy Bill Nenga,” anasikika akisema TID kwenye video hiyo kabla ya washkaji zao kudakia mazungumzo hayo kwa kutajataja jina la rapper huyo.
Miezi kadhaa iliyopita, TID alilalamika kuwa Bill ni mtu mwenye tamaa na asiye na shukrani baada ya kuondoka Radar Entertainment licha ya kumlea na kumfikisha pahali.
“Mimi sikuwa na mkataba na Billnass,” alisema TID kwenye interview moja. “Mkataba wangu ulikuwa ni maneno tu kwamba namsaidia na yeye alikuwa na nia sana kwamba anataka kusaidiwa, nimemsaidia kwenye wimbo wa kwanza, nimelipia gharama zangu kwenye video pia, hadi hoteli chakula chake, kila kitu mimi nimefanya lakini kitendo cha kutoka bila kuniambia mimi halafu baadaye ananipigia simu kwamba ‘mzee hii ni stunt tu nimetengeneza kwamba mimi nimeondokana na Radar lakini hiyo sio kweli baadaye nitakanusha.’ Kweli hivyo vitu na akili yako unaweza kufanya kwa mtu ambaye anakusaidia? Mimi kwakweli Billnass amenikasirisha sana na sitaki aniharibie kwasababu anaonekana ni mtu mwenye tamaa tu ya kutaka vitu fulani,” aliongeza TID.
Katika muda wote huo Bill hakuwahi kumjibu vibaya TID na aliendelea kusisitiza kuwa ni mtu anayemshukuru kwa msaada aliompa.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi