,./.,

,,

... ...

';';';';

..,,..

''=

==

\\..\\

Drop Down MenusCSS Drop Down MenuPure CSS Dropdown Menu

Tuesday, October 18, 2016

Kama ulishtushwa au kushangazwa au pengine ulikerwa na mistari ya Nay wa mitego enzi anatoka basi ujue haupo peke yako. Hata producer aliyeutengeneza wimbo huo aliuponda.

Nay ameiambia Planet bongo ya EA Radio kuwa wimbo wake wa kwanza “Wamitego” beat yake ilitengenezwa na P-funk lakini alipousikiliza wimbo kabla haujatoka alimwambia nay kwanini ametumia beat yake kali kuimba maneno ya kipuuzi?
majani187-20161015-0001
P-funk Majani
Nay anasema hiyo ilimkata stimu akihisi amekosea sana na sababu kubwa ni kuwa P funk alikuwa anajua wakati nay hakuwa na mahusiano mazuri na mama yake mzazi wakati anarekodi huo wimbo lakini akamshauri kuwa hayakuwa maamuzi mazuri kumponda mzazi kwenye wimbo hata kama amekosea.
Hata hivyo aliamua kuuchukua wimbo huo na kumpelekea mmoja wa madj wa radio moja hapa bongo (hakumtaja) ambaye alimwambia ni kali na hapo ukawa mwanzo wake kutoka.
Nay amesema anazo ngoma zaidi ya 6 alizofanya Bongo records kwa majani lakini hakuwahi kupewa hadi leo sababu zikiwa ni kama hizo za kuimba kile P funk alichokiita “Upuuzi”.
Hata hivyo nay anasema maisha yake binafsi ndiyo yamempa ujasiri wa kusema chochote bila kuhofia lolote na hii ni tabia yake halisi na ameamua kuchukua maisha yake kuyahamishia kwenye Rap.

0 comments:

Post a Comment

ufunguzi